Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:58

Wahamiaji 18 wafariki walipojaribu kuvuka mpaka wa Morocco kuingia Uhispania


Wahamiaji kutoka Morocco wakijaribu kuingia Uhispania kwenye mpaka wa Melilla
Wahamiaji kutoka Morocco wakijaribu kuingia Uhispania kwenye mpaka wa Melilla

Darzeni za watu wamepigwa pichwa wakiwa wamelala kwenye uzio wa  mpaka wa Morocco, wengine wakiwa wanavuja damu na wengine hawajiwezi, katika video inayoonyesha matokeo ya wahamiaji kuvuka katika eneo na Uhispania siku ya Ijumaa ambapo watu takriban 18 walikufa.

Mamlaka za Morocco zimesema kwamba janga hilo lilitokea baada ya wahamiaji kujaribu kuvamia mpaka kwenye eneo la Melilla . Wengine walifariki kutokana na mkanyagano na wengine kuanguka kutoka kwenye uzio huo.

Picha hizo zimebandikwa katika mtandao wa facebook na kitengo cha shirika la haki za binadamu ambacho kinafanyakazi na wahamiaji ikiwemo karibu na Melilla. Mkuu wa kitengo hicho Omar Naji ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba picha za video zimechukuliwa na wajumbe wa jumuiya hiyo na watu waliohuzunishwa na tukio hilo.

Mapema Ijumaa asubuhi takriban wahamiaji 2,000 walijaribu kuvamia uzio wa eneo la Uhispania na kusababisha mapigano makali na vikosi vya usalama vya Morocco na Uhispania. Takriban watu 100 waliweza kuvuka.

XS
SM
MD
LG