Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:39

Tanzania yaanzisha operesheni dhidi ya wahamiaji haramu katika eneo la Loliondo


Mtetezi wa haki za Wamasai akikamatwa wakati wa maandamano mjini Nairobi, ya kupinga kuondolewa kwa jamii ya Masai katika hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania, June 17, 2022. Picha ya AFP
Mtetezi wa haki za Wamasai akikamatwa wakati wa maandamano mjini Nairobi, ya kupinga kuondolewa kwa jamii ya Masai katika hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania, June 17, 2022. Picha ya AFP

Tanzania Jumatano imesema itakabiliana na wamahiaji haramu katika eneo la kaskazini mashariki la Loliondo, ambako inadaiwa kuwa wafugaji Wamasai wa Kenya wanaunga mkono wanaopinga mpango wa kutenga eneo la ulinzi wa wanyamapori.

Wamasai wa Loliondo wameishtumu serikali ya Tanzania kujaribu kuwaondoa kwa nguvu kwenye ardhi yao ili kuandaa utalii na mashindano ya uwindaji.

Lakini serikali ilitupilia mbali tuhuma hizo, ikidai kwamba inataka kulinda ardhi ya kilomita mraba 1,500 ili isiharibiwe na shughuli za binadamu. Inasema ni sehemu ndogo ya eneo ambalo linachukua kilomita mraba 4,000 karibu na mpaka wa Kenya.

Mvutano juu ya mradi huo ulisababisha kifo cha askari polisi mmoja wakati wa maandamano ya tarehe 10 mwezi huu, baada ya wafanyakazi kujitokeza na kuweka mipaka ili kutenganisha eneo la kulindwa.

“Kufuatia maelekezo ya waziri wa mambo ya ndani, tutaendesha operesheni kwa siku 10 dhidi ya wahamiaji haramu pembeni mwa Loliondo na wilaya ya Ngorongoro,” Kamishna mkuu wa idara ya uhamiaji, Anna Makakala, amesema Jumatano.

XS
SM
MD
LG