Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:16

Wahamiaji 17 kutoka Haiti wafariki baada ya boti yao kuzama


Wahamiaji kutoka Haiti, waliorejea kwenye eneo la mpakani la Mexico keupuka kurudishwa nchini mwao, Septemba 25, 2021. Picha ya Reuters
Wahamiaji kutoka Haiti, waliorejea kwenye eneo la mpakani la Mexico keupuka kurudishwa nchini mwao, Septemba 25, 2021. Picha ya Reuters

Watu 17 walifariki baada ya boti iliyokuwa inabeba darzeni ya wahamiaji wa Haiti kuzama kwenye pwani ya kisiwa cha Bahamas, maafisa wamesema Jumapili, wakati raia wengi wa Haiti wanajaribu kufika Marekani wakikimbia ghasia za magenge yenye silaha na umaskini nchini mwao.

Timu za uokoaji ziliopoa miili ya watu 17, akiwemo mtoto mchanga, na watu 25 waliokolewa, waziri mkuu wa Bahamas Philip Davis aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Davis alisema maafisa wanaamini watu hao walikuwa kwenye boti ya mwendo kasi kuelekea Miami.

“Inaaminika kuwa boti hiyo ilizama kwenye bahari iliyochafuka”, amesema.

Hadi watu 60 walikuwa kwenye boti hiyo na watu zaidi wanahofiwa kutoweka, Kamishna wa polisi Clayton Fernander amesema.

Maafisa wa Bahamas wamesema watu wawili wamekwa mbaroni, wote ni kutoka Bahamas, wakishukiwa kufanya usafirishaji haramu wa binadamu. Watu wote waliokuwa kwenye boti ambao waliokolewa au kufariki au waliotoweka wanaaminika kuwa wahamiaji kutoka Haiti.

Waziri wa idara ya uhamiaji Keith Bell amesema manusura walieleza kuwa walilipa kati ya dola 3,000 na dola 8,000 kwa safari hiyo.

XS
SM
MD
LG