“Walinzi wa pwani wa jeshi la majini wakiwa kwenye doria baharini katika bahari ya Mediterania na Atlantic, waliwaokoa watu 257 waliokuwa wakijaribu kufanya uhamiaji haramu, baada ya kujaribu kuvuka katika hali hatarishi kwenye boti za kienyeji, boti za mashindano kwenye maji, hata kuogelea,” amesema afisa wa jeshi ambaye jina lake halikutajwa, akinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Morocco MAP.
Wahamiaji wengi ni kutoka mataifa ya Afrika, lakini walikuwemo pia kutoka Afghanistan na Yemen, MAP imeripoti, ikiongeza kuwa walifikishwa kwa usalama ufukweni.
Miongoni mwa wahamiaji hao walikuwemo wanawake na watoto pia.
Mwezi uliopita, wahamiaji 23 walifariki wakijaribu kupanda uzio wa mpaka ndani ya eneo la Uispania la Melilla, kwenye pwani ya Mediterania ya Morocco.
Zaidi ya wahamiaji 40,000, wengi kutoka Morocco, waliwasili Uispania mwaka wa 2021 kwa njia ya bahari, kwa mujibu wa wizara ya Uispania ya mambo ya ndani.