Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:58

Watu 168 hawajulikani walipo, 8 wameuawa Nigeria.


Gari moshi linalosafiri kutoka Abuja hadi Kaduna. Picha: AFP
Gari moshi linalosafiri kutoka Abuja hadi Kaduna. Picha: AFP

Shirika la usafiri wa reli nchini Nigeria limesema kwamba zaidi ya abiria 168 hawajulikani walipo kufikia sasa, wiki moja baada ya treni waliokuwa wanasafiria kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Watu wanane waliuawa na wengine hawajulikani walipo tangu march 28, washambuliaji walipolipua bomu na baadaye kuanza mashambulizi ya risasi, katika treni inayokuwa ikielekea mji mkuu wa Abuja kutoka Kaduna, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kwamba baadhi ya abiria walitekwa nyara.

Walionusurika tukio hilo walisema kwamba watu waliokuwa wamejihami wa bunduki waliteka nyara baadhi ya abiria bila kujua idadi kamili ya abiria waliotekwa nyara.

Shirika la reli nchini Nigeria limesema kwamba kati ya abiria 176, na watu 8 wamethibitsihwa kuuawa na 168 hawajulikani walipo kabisa.

Taarifa ya shirika hilo imesema kwamba juhudi zinaendelea kuwaokoa abiria hao huku sehemu ya reli iliyoharibiwa ikitengenezwa.

XS
SM
MD
LG