Buhari, ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2015, alitumia wiki kadhaa kujadiliana na magavana wa majimbo na wajumbe wa chama ili kushinikiza msimamo wa makubaliano kabla ya kongamano siku ya Jumamosi.
Jumamosi usiku chama kilikubali Abdullahi Adamu, seneta ambaye alikuwa akiungwa mkono na Buhari ili kuepusha mizozo zaidi, kulingana na kamati ya uchaguzi ya chama cha All Progressives Congress (APC).
Ushindani wa kisiasa tayari umeanza kuchukua nafasi ya Buhari kama kiongozi wa taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika lakini kinyang'anyiro hicho kimesalia wazi huku vigogo kadhaa wakichuana.