Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 00:00

Chama tawala Nigeria kimefanya kongamano la kumchagua mwenyekiti mpya

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hatagombea katika uchaguzi ujao wa mwaka 2023 akiwa anamaliza muhula wake wa pili.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hatagombea katika uchaguzi ujao wa mwaka 2023 akiwa anamaliza muhula wake wa pili.

Chama tawala nchini Nigeria kimefanya kongamano lake la kitaifa Jumamosi kumchagua mwenyekiti mpya na kuondokana na mizozo kabla ya kumchagua mgombea atakayechukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari katika uchaguzi ujao wa mwaka 2023.

Mkutano wa Abuja unalenga kumaliza mabishano ya ndani ambayo Buhari alionya kuwa yanaweza kuharibu umoja wa chama na mafanikio yake katika kura.

Mbinu za kisiasa zinazidi kupamba moto kutafuta kuchukua nafasi ya Buhari kama kiongozi wa taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika lakini kinyang'anyiro hicho kiko wazi huku vigogo kadhaa wakichuana kuwania nafasi hiyo.

Viongozi na wajumbe wote wa chama cha Progressives Congress (APC) wanakutana ili kuchagua mwenyekiti mpya na nyadhifa nyingine katika hatua ya mwisho kabla ya mchujo baadaye mwaka huu wa mgombea wa urais.

XS
SM
MD
LG