Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 17:29

Je, China inaweza kuihami Afrika kuepuka athari za vikwazo alivyowekewa Russia?


Watu waliolazimika kuhama makazi yao wakiwa mjini Bor, Sudan Kusini wakipokea msaada mwezi uliopita. (Kate Bartlett/VOA)

Warefu, wenye kujiheshimu na wakiwa wamevaa nguo zenye rangi zilizokoza za kipekee katika ardhi kavu, wanawake wakiwa katika eneo la Umoja wa Mataifa la usambazaji chakula katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini, wanasubiri kwa utulivu katika mstari huku kukiwa na joto kupokea resheni zao za chakula za kila mwezi.

“Maisha yangu yalibadilika tangu [Sudan Kusini 2011] ilipopata uhuru. Hivi sasa napata msaada – hali imekuwa afadhali,” Rebecca Akeer, mwenye umri wa miaka 50, alisema akiwa nje ya nyumba yake ya matope wakati wafanyakazi wa misaada wakikabidhi magunia makubwa ya nafaka.

Lakini Akeer na wenzake katika nchi ya Afrika iliyokumbwa na vita angeweza hivi karibuni kushuhudia athari za vita vya mbali vya Ulaya vikipiga hodi, huku wachambuzi wakiwaza iwapo China inaweza kuzuia athari inayotarajiwa ya vikwazo vya kimataifa dhidi ya Russia kwa bara la Afrika.

Ukosefu wa Chakula

Mzozo wa Ukraine na vikwazo ilivyowekwa Russia vimeleta ongezeko la bei ya mafuta na chakula ulimwenguni, ambapo vinaweza kupelekea njaa zaidi Afrika, na hata machafuko zaidi, wachambuzi wanasema.

“Tunaelekea katika vurugu,” alisema Steven Gruzd, mtaalam wa Russia na mchambuzi wa sera za mambo ya nje katika Taasisi ya Masuala ya Kimataifa huko Johannesburg, Afrika Kusini.

“Bei ya mkate inaongezeka. Wakati mwingine inasababisha watu waingie mitaani,” aliongeza, akieleza kuwa mapinduzi katika nchi jirani ya Sudan kimsingi yalianza kwa machafuko ya bei ya mkate 2018.

“Nafikiri ukosefu wa usalama wa chakula utakuwa na matokeo makubwa kwa vita hii.”

Russia ni muuzaji mkubwa wa nje wa ngano, na Ukraine ni ya tano kwa usafirishaji huo. Nchi za Kaskazini mwa Afrika, kama vile Misri mshirika mkuu wa kibiashara wa Russia huko Afrika, wanatarajiwa kuhisi athari za vikwazo hivyo. Tunisia imesema tayari inatafuta kwingine atakaye wauzia ngano.

“Wakati tukiangalia athari za vita vya Ukraine katika usalama wa chakula duniani, katika mwaka wa mahitaji ya kibinadamu yaliyokuwa hayajawahi kutokea, WFP ina wasiwasi mkubwa wakati vita hivi vinaweza kuwa na athari kubwa zaidi,” Claudio Altorio, msemaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, ameiambia VOA.

Watu waliolazimika kuhama makazi yao wakiwa mjini Bor, Sudan Kusini wakipokea msaada wa chakula mwezi uliopita. (Kate Bartlett/VOA)
Watu waliolazimika kuhama makazi yao wakiwa mjini Bor, Sudan Kusini wakipokea msaada wa chakula mwezi uliopita. (Kate Bartlett/VOA)

Shughuli za Russia chini ya Rais Vladimir Putin ziliongezeka kwa haraka Afrika katika muongo uliopita. Kukabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya, Vladimir Padalko, makamu rais wa Baraza la Russia la Biashara na Viwanda, amesema Moscow ilipanga kuongeza vituo vyake vya biashara Afrika kama ni mbadala kwa bidhaa kama vile matunda, chai na kahawa, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Russia Tass.

Russia imejihusisha na mataifa yenye historia ya kutokuwa na utulivu kama vile Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako ina maslahi ya madini, na ambapo wakandarasi binafsi wa kijeshi wenye makao yao Russia wanaendesha shughuli zao.

Mwaka 2021, jumla ya mahusiano ya pande mbili ya kibiashara kati ya China na Afrika yalifikia thamani ya dola bilioni 254.3, mamlaka za China zimesema. Kinyume chake, biashara ya Russia na Afrika ilikuwa na thamani ya takriban dola bilioni 20, kulingana na benki ya Afrika ya Exim.

“Ukubwa wa biashara ya China na Afrika tayari ni mara 10 au zaidi kwa ukubwa kuliko biashara ya Russia na Afrika,” amesema Gruzd. “Iwapo njia za upelekaji zikipungua, China huenda ikawa na nafasi nzuri kuchukua nafasi hiyo.”

Cobus van Staden, mtafiti mwandamizi wa masuala ya China na Afrika katika Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Afrika Kusini, inaona uwepo wa fursa pia ya maslahi ya nchi kuu za Afrika zinazofanya biashara nje.

“Nchi za Afrika kwa ujumla zinajaribu kuongeza usafirishaji nje wa mazao ya kilimo kwenda China. Afrika Kusini inasafirisha bidhaa zaidi China na Russia … hivyo kampuni za Afrika Kusini zinaweza kuitegemea China kujaza pengo hili,” alisema.

Lakini Wandile Sihlobo, mchumi mwandamizi katika baraza la biashara ya kilimo Afrika Kusini, alisema hafikirii kuwa vikwazo dhidi ya Russia vitaongeza biashara kati ya China na Afrika. Anasema anafikiria Umoja wa Ulaya, Marekani na Canada watakuwa na fursa zaidi kuiuzia Afrika nafaka na kwa kwango fulani, mafuta.

“China kwa kweli haina bidhaa za kusafirisha nje kama vile mafuta na nafaka ambazo nchi za Kiafrika kwa kweli zinahitaji. … Hata hivyo ni kati ya wazalishaji wakubwa wa nafaka, wanazalisha zaidi kwa ajili ya matumizi yao wenyewe,” alisema.

China imekuwa na msimu mbaya hasa wa upandaji. Wiki iliyopita, waziri wa kilimo wa China alisema zao la ngano la kipindi cha baridi linaweza kuwa “baya zaidi katika historia.” Bei tayari zimepanda kwa sababu ya mzozo wa Ukraine.

Nishati ya Afrika

Wakati usalama wa chakula utawaumiza Waafrika wa hali ya chini zaidi, mifuko ya baadhi ya nchi za Kiafrika zenye utajiri wa mafuta kuna uwezekano wa kunufaika kutoka na kusitishwa kwa mafuta na gesi ya Russia.

“Wazalishaji wa mafuta [Afrika] kwa kipindi kifupi wanaweza kupata manufaa kwa kiasi fulani,” Gruzd alisema.

Van Staden alisema kuwa manufaa yanaweza kuongezeka hata zaidi iwapo China itashirikiana kutekeleza vikwazo vya kimataifa dhidi ya Russia, kitu ambacho bado hakijatokea.

Jukwaa linaloelea la uchimbaji mafuta la Kaombo Norte la nje ya pwani ya Angola lilipigwa picha kutoka katika Helikopta, Nov. 8, 2018. REUTERS/Stephen Eisenhammer - RC1BBCE4AC60
Jukwaa linaloelea la uchimbaji mafuta la Kaombo Norte la nje ya pwani ya Angola lilipigwa picha kutoka katika Helikopta, Nov. 8, 2018. REUTERS/Stephen Eisenhammer - RC1BBCE4AC60

“Iwapo hali itakuwa kwamba wao [China] wanasimamia kuzuia usafirishaji nje wa mafuta na gesi ya Russia, wazalishaji wa mafuta na gesi Afrika wanaweza kuwa maslahi ya muda mfupi,” alisema, akiongeza, “Kuna uwezekano wa kuiona China ikinunua mafuta zaidi kutoka Angola, na kuna mlolongo wa miradi ya gesi asilia inayoanza kujitokeza nchini Tanzania.”

“Kwa upande wa China, wao ni uchumi mkubwa na kuongeza vyanzo vyao vya bidhaa ni mkakati wao katika hali yoyote ile,” alisema van Staden. “ Hivi ndiyo China ilianzisha mradi wa Belt and Road Initiative.”

Kubadilisha Washirika

Kabla ya kuanguka kwa Umoja wa Soviet, nchi nyingi za Kiafrika zilionekana ama ziko chini ya himaya ya ushawishi wa Washington au Moscow, mgawanyiko ambao baadhi ya wachambuzi wanaamini unaweza ukarejea kutokana na vita hii ya Ukraine.

“Maeneo ya kubahatisha ninayoona ni kwa serikali za Afrika zinaweza kuhisi kuna ulazima wa ‘kuchagua upande’wa kuegemea katika hali mpya ya Vita Baridi,” alisema Yunnan Chen, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Kinacho Jishughulisha na Tafiti za China na Afrika.

“Tumeona mgawanyiko mkubwa katika hilo kwa Afrika Kusini na BRICS [Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini] kwa upande mmoja na Kenya kwa upande mwingine,” ameongeza, akieleza kujizuia kwa Afrika Kusini katika kupigia kura wiki iliyopita azimio la UN likiitaka Russia kuondoka Ukraine (China pia ilijizuilia).

Kinyume chake, Kenya na Nigeria zilionyesha kuiunga mkono Ukraine na kuilaani Moscow.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG