Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:25

5 Wafariki katika ajali ya ndege Sudan kusini


Mji wa Juba

Watu 5 wamefariki katika ajali ya ndege nchini Sudan kusini.

Ndege ndogo ya kubeba mizigo inayosimamiwa na shirika la Optimum, imeanguka mda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Juba.

Maafisa katika uwanja huo wameanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Juba amesema kwamba ndege hiyo ya Antonov-26, ilikuwa imebeba mapipa ya mafuta kutoka Juba kuelekea Maban, jimbo la Upper nile.

Waliokufa walikuwa wafanyakazi wa ndege hiyo.

Sudan kusini, ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa mda wa mwongo mmoja sasa, haina mfumo wa kutegemewa wa usafiri kwa njia ya barabara, hali inayolazimu baadhi ya mizigo kusafirishwa kwa ndege.

XS
SM
MD
LG