Upatikanaji viungo

Breaking News

Uhalifu wa kimitandao watumika kabla ya Kashoggi kuuwawa


Jamal Khashoggi

Watafiti ambao waliripoti kuwa programu ya kijasusi iliyotengenezwa na kampuni ya Israeli ilitumika kufanya ujasusi dhidi ya marafiki wa karibu wa Jamal Khashoggi kabla ya mauaji ya kinyama aliyofanyiwa na sasa wanalengwa na majasusi wa kimataifa, Shirika la habari la Associated Press limegundua.

Mbinu za ujasusi zafichuliwa

Mara mbili mwezi uliopita, watu wanaojifanya kuwa wao ni wawekezaji wa harakati za muamko wa kijamii wamekuwa wakiwashawishi wanachama wa kikundi kinacho fuatilia mitandao ya kijamii maarufu kama Citizen Lab internet watchdog kuhudhuria mikutano katika hoteli za kifahari kuwauliza kwa saa kadhaa juu ya kazi yao ya kuujulisha umma juu ya ujasusi unaofanywa na Israeli na kuchukua maelezo ya kina kuhusu maisha yao binafsi. Katika hali zote mbili, watafiti hao wanaamini watu hao wakati wa mazungumzo hayo walirikodiwa kwa siri.

Mkurugenzi wa Citizen Lab Ron Deibert ameeleza mbinu hizi kama “ni kitendo cha kujishusha hadhi kilicho kuwa hakitarajiwi kilicho vunja rikodi.”

“Tunalaani vitendo hivi viovu, vya ulaghai kwa kemeo kali kabisa,” amesema katika tamko lake Ijumaa.

“Kitendo hiki cha ulaghai dhidi ya kikundi cha wanazuoni kama hawa wa Citizen Lab ni shambulizi kwa uhuru wa wanazuoni wote.”

Bado ni kitendawili hawa majasusi wanafanya kazi kwa niaba ya nani, lakini mbinu zao zinakumbusha mbinu za wachunguzi wakujitegemea ambao hutumia utambulisho wa uongo kutafuta habari za kijasusi au kutafuta nyaraka zitakazo wadhibiti watu wanao wakosoa viongozi wenye madaraka katika serikali au biashara.

Citizen Lab imekuwa mstari wa mbele

Citizen Lab, ambayo iko katika chuo cha masuala ya kimataifa (Munk School of Global Affairs ) huko chuo kikuu cha Toronto, kwa miaka kadhaa kimekuwa mstari wa mbele kuwafichua wadukuzi wanaosaidiwa na serikali ambao wanaendesha shughuli zao katika maeneo ya mbali kama vile Tibet, Ethiopia na Syria.

Hivi karibuni kikundi hicho kimepata umashuhuri kwa kuendelea kufichua mbinu za programu ya ujasusi ya kampuni moja ya Israeli ijulikanayo kama NSO Group, ambapo bidhaa zake za kieletroniki zimetumika na serikali kuwafuatilia waandishi wa habari Mexico, viongozi wa upinzani huko Panama na wanaharakati wa haki za binadamu huko Mashariki ya Kati.

Mwezi Octoba, Citizen Lab imeripoti kuwa simu aina ya IPhone ya moja wa wandani wa Khashoggi ilishambuliwa na virusi vya kijasusi vinavyo tengenezwa na kampuni ya NSO Group miezi michache kabla ya Khashoggi kuuwawa kikatili.

Rafiki huyo, ambaye ni mpinzani wa Saudi Arabia Omar Abdulaziz, baadae alidai kuwa udukuzi huo uliwapa fursa majasusi wa Utawala wa Saudi Arabia kujua ukosoaji aliyokuwa anaufanya Khashoggi yeye binafsi dhidi ya Familia ya Kifalme na “lilichangia kwa kiwango kikubwa” juu ya mauaji yake.

NSO yakanusha tuhuma za ujasusi

Katika tamko lake, kampuni ya NSO ilikanusha kuwa kwa namna yoyote ile inahusika na operesheni ya ujasusi huo unaolenga wanazuoni na watafiti wa Citizen Lab, “kwa kuhusika moja kwa moja au njia yeyote nyingine” na kusema kwamba haijawahi kuajiri wala kumtaka mtu yeyote kuwaajiri wachunguzi binafsi kuifuatilia taasisi hiyo ya Canada, Citizen Lab.

“Shutuma zozote kinyume cha maelezo yao hazina ukweli na si kingine bali ni dhana zisizo kuwa na msingi,” NSO imesema.

NSO kwa muda mrefu imekuwa ikikanusha kuwa programu yake ya ujasusi wa mitandao ili tumika kumlenga Khashoggi, japokuwa imekataa kutamka ilipo ulizwa iwapo kwa upana zaidi imeuza programu hiyo kwa serikali ya Saudi Arabia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG