Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:24

Mfalme Salman apongeza mahakama iliyosikiliza kesi ya Khashoggi


Prince Mohammed bin Salman
Prince Mohammed bin Salman

Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia ameipongeza mahakama na Wizara ya Sharia ya nchi yake katika hotuba yake ya kwanza tangu kuuliwa kwa mkosowaji mkuu wa serikali Jamal Khashoggi.

Matamshi yake yametolewa siku chache tu baada ya shirika la kijasusi la Marekani, CIA, kutoa tamko kuwa mwanawe Mohamed ndiye aliye amrisha mauaji hayo, shutuma ambazo zimeitumbukiza taifa hilo la kifalme katika mzozo mkubwa wa kimataifa ambao haujawahi kutokea.

Akitoa hotuba yake ya kila mwaka mbele ya baraza kuu la ushauri (Shuraa) hii Jumatatu Mfalme Salman, alipongeza mfumo wa sharia ulioko nchini mwake.

Ufalme wa Saudi Arabia

"Taifa hili la kifalme limeundwa chini ya mfumo wa misingi ya sharia za Kiislamu na usawa na tunapongeza juhudi za mahakama na mwendesha mashtaka wa serikali katika kufanya kazi kuhakikisha misingi hiyo inaheshimiwa," amesema Salman.

Wiki iliyopita mwendesha mashtaka wa serikali ya Saudi Arabia alifutilia mbali tuhuma zote dhidi ya mwanamfalme menye ushawishi mkubwa Mohamed Bin Salman anaye husishwa na mauaji ya mwandishi wa habari Khashoggi aliyeuliwa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul oktoba 2.

Na mwendesha mashtaka alipendekeza hukumu ya kifo kwa watu watano alipokuwa anatangaza kuwafungulia mashtaka watu 11 anaosema walihusika moja kwa moja na mauaji yake. Kwa ujumla anasema kuwa watu 21 wanashikiliwa kuhusiana na kadhia hiyo.

Mfalme Salman mwenye umri wa miaka 82 hakuzungumzia moja kwa moja mauwaji ya mwandishi huyo wa Washington post wakati wa hotuba yake.

Hata hivyo shirika la kijasusi la Marekani CIA kupitia ripoti za vyombo vya habari linaamini Mwanamflame Mohamed ndiye aliamrisha mauaji ya khashoggi.

Lakini Rais Donald Trump hadi hivi sasa hajaunga mkono matokeo ya CIA na akijibu maswali ya waandishi wa habari mwishoni mwa wiki hakutaka kusema nani alihusika.

Trump kupokea ripoti

Tutakuwa na ripoti kamili juu ya suala hilo mnamo siku mbili zijazo labda Jumatatu au Jumanne. Na CIA haijatathmini chochote. Ni mpama mno ni ripoti iliyotolewa mapema. Lakini inawezakena hali hiyo ilitokea tutaangalia zaidi.

Akizungumza na shirika la habari la Fox Jumapili Rais Trump alisema kwamba mwanamflame alimueleza mara tano kwamba hajahusika na mauwaji ya khashoggi.

Licha ya kauli hiyo wabunge wa chama cha Demokrats wanamhimizaTrump kukubali uamuzi ulofikiwa na idara za ujasusi za Marekani. Na Warepublikan wanasisitiza watu wawe na subra huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ikisisitiza kuwa hakuna uamuzi wa mwisho ulofikiwa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG