Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 13:59

Uturuki yatuma ushahidi rikodi za mauaji ya Khashoggi kwa mataifa 5


Rais Recep Tayyip Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumamosi ametuma yale yaliyo kuwa yamerikodiwa katika kifo cha mwandishi wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi kwa nchi tano; Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Saudi Arabia na Marekani.

Hata hivyo hakukuwa na taarifa za papo hapo zinazothibitisha kuwa nchi hizo tano zilikuwa zimepokea rikodi hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema mapema wiki hii serikali yake inazo taarifa zaidi kuhusiana na mauaji haya na kuna uwezekano mkubwa itaweka hadharani ushahidi huu baada ya uchunguzi wa kifo cha Khashoggi kukamilika.

Akizungumza wakati wa ziara yake Japan, Cavusoglu amewaambia waandishi wa habari kuwa Uturuki imesema Saudi Arabia na nchi nyingine ambazo zina maslahi na ripoti hizi wamepewa fursa ya kuziona.

Khashoggi aliuwawa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko mjini Istanbul Octoba 2.

Hapo awali, Saudi Arabia ilisema Khashoggi alikuwa ameingia katika ubalozi huo na kuwa taarifa za alikokwenda hazijulikani, lakini baadae walisema alikufa katika mapigano ya kurushiana ngumi na hatimaye wakasema alikufa kwa kupigwa kabari.

Mwendesha mashtaka wa Ufalme huo tangu wakati huo ameyaita mauaji hayo yalipangwa, lakini hakueleza nani aliyekuwa ameyapanga au kuyaidhinisha.

XS
SM
MD
LG