Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 09:16

Trump asema huenda wahuni walio muua mwandishi wa Saudia


Waandishi wa habari wakiripoti yanayojiri nje ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia juu ya kutoweka kwa mwandishi wa Saudia Jamal Khashoggi Octoba 14, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump anaamini mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi aliye toweka yapata wiki mbili zilizopita, huenda wahuni walio muua.

Khashoggi alitoweka tangu Oktoba 02 baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki.

Trump amesema Jumatatu amefanya mazungumzo ya simu kwa dakika 20 na Prince wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ambaye amemwambia kwamba haana taarifa yoyote kuhusu kilichomtokea Khashoggi.

Rais alimtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje Mike Pompeo mjini Riyadh kufanya mazungumzo na mfalme Salman kuhusu kutoweka kwa Khashoggi.

Khashoggi aliingia katika ubalozi mdogo Octoba 2 ili kuchukuwa makaratasi yake aliyokuwa anayahitaji ili kumwezesha kufunga ndoa na mchumba wake, Hatice Cengiz, raia wa Uturuki ambaye alisubiri ndani ya gari nje ya jengo la ubalozi lakini hakumuona tena Khashoggi.

Jioni Jumapili, Ufalme wa Saudia na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan walijadili juu ya kuunda kikosi kazi cha pamoja kuchunguza kupotea kwa Khashoggi, ambapo maafisa wa Uturuki wanaamini aliuwawa na majasusi wa Saudia ndani ya Ubalozi.

Saudi Arabai imesema madai hayo “hayana msingi” na kusema Khashoggi aliondoka Ubalozini kwa hiari yake, japokuwa siyo Uturuki wala Saudi Arabia imetoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha maelezo yao kuhusiana na tukio hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG