Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:52

Trump : 'Serikali itatoa ripoti ya mauaji ya Khashoggi Jumanne'


Rais Donald Trump akiwasili California
Rais Donald Trump akiwasili California

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Jumamosi kuwa bado serikali haijafikia uamuzi wa mwisho juu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi.

Uongozi wa Trump umesema hauna uhakika juu ya ripoti ambayo kwa maelezo ya Shirika la Kijasusi la Marekani, kwamba Prince Mohammed bin Salman aliagiza Khashoggi auwawe, ambaye alikuwa ni mwandishi wa makala zilizokuwa zikichapishwa na gazeti la Washington Post. Wizara ya Mambo ya Nje imetaja kuwa ripoti hizo "sio sahihi."

Mkurugenzi wa CIA Gina Haspel na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo walimpa taarifa Rais Donald Trump juu ya suala la Khashoggi katika mazungumzo ya simu Jumamosi wakati rais akiwa anaelekea California.

Baadae, wakati anatembelea maeneo yaliyo kuwa yameathiriwa na moto wa misituni upande wa Kusini mwa California, Trump amewaambia waandishi kuwa serikali ya Marekani itatoa ripoti yake Jumanne kueleza nani aliyemuuwa Khashoggi.

Tamko kutoka Wizara ya Mambo ya Nje lilitolewa dakika chachew baada ya msemaji wa rais Sarah Sanders kusema kuwa Trump " ana imani na CIA."

Kabla ya Rais Donald Trump kuondoka Washington Jumamosi alisema kuwa bado hajapatiwa taarifa zozote juu ya ripoti ya Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) inayotoa majumuisho kuwa Prince wa Saudia Mohammed bin Salman aliamrisha mwandishi wa Saudi Arabia kuuwawa, lakini atapewa taarifa hizo baadae siku ya leo.

“Tutakuwa na mazungumzo na CIA baadae na mambo mengine mengi. Nitafanya hilo wakati nikiwa ndani ya ndege safarini,” Trump aliwaambia waandishi White House kabla ya kuondoka kuelekea California. “Pia nitakuwa namazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo.”

CIA imeeleza inaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman ndiye aliye amuru kuuwawa kwa mwandishi wa habari huyo Jamal Khashoggi, raia wa Saudi Arabia.

Tathmini ya CIA ambayo awali iliripotiwa na gazeti la Washington Post Ijumaa, inakinzana na ile iliyotolewa na Saudi Arabia, ambayo mwendesha mashtaka mkuu siku moja kabla ya kutolewa tathmini hiyo ilimsafisha Prince Mohammed bin Salman kuhusika na mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa CIA ilikuwa imefikia majumuisho ya mwisho kuwa majasusi 15 wa Saudi Arabia walikwenda Istanbul kwa kutumia ndege ya serikali na kumuuwa Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudia.

XS
SM
MD
LG