Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:16

Afisa wa Saudia : Kilicho muuwa Khashoggi ni kabari


Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Wakati kauli ya Saudi Arabia ikiendelea kutiliwa mashaka kimataifa juu ya taarifa ya kifo cha mwandishi Jamal Khashoggi, afisa wa ngazi ya juu wa serikali hiyo ametoa tamko jipya la kifo cha mwandishi huyo akiwa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia huko Istanbul, ambazo zinakinzana na maelezo yaliyotolewa awali.

Maelezo ya hivi karibuni yaliotolewa na afisa wa Saudia ambaye hakutaka jina lake litajwe, ni pamoja na ufafanuzi kuhusu kikundi cha raia 15 wa Saudia waliopelekwa kupambana na Khashoggi Octoba 2, kwa vitisho vya kumpa madawa ya kupoteza fahamu na kumteka na baadae kumkaba hadi akafa wakati alipokuwa akipambana nao.

Baada ya hapo mmoja kati ya wana kikundi hao alivaa nguo za Khashoggi ionekane kama kwamba alikuwa ameondoka ubalozini.

Baada ya kukanusha kuhusika na kutoweka kwa Khashoggi, 59, kwa wiki mbili, Saudi Arabia Jumamosi asubuhi ilisema kuwa alikuwa amekufa kutokana na mapigano ya kutupiana ngumi yaliotokea ubalozini. Saa moja baadae, afisa mwengine wa Saudia alieleza kifo chake kilitokana na kukabwa, jambo lililosisitizwa na afisa wa ngazi ya juu.

Maafisa wa Uturuki wanashuku kuwa mwili wa Khashoggi, mwandishi wa safu maalum katika gazeti la Washington Post na mkosoaji mkuu wa Prince Mohammed bin Salman, mwili wake ulikatwa vipande vipande, lakini afisa wa Saudia amesema ulikuwa umefungwa katika zulia na kukabidhiwa kwa “msaidizi ndani ya Uturuki” ili akautupe.

Alipoulizwa kuhusu tuhuma kwamba Khashoggi alikuwa ameteswa na kukatwa kichwa, afisa huyo alisema uchunguzi wa awali hauonyeshi hilo.

Afisa wa Saudia ameeleza kile alichosema kuwa ilikuwa ni nyaraka za idara ya usalama wa ndani ya Saudia zinaonyesha kulikuwa na hima ya kuwarejesha wapinzani wote nchini na pia mpinzani maalum ikiwa ni Khashoggi.

XS
SM
MD
LG