Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:14

Wahusika mauaji ya Khashoggi watachukuliwa hatua anasema Pompeo


Mike Pompeo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Mike Pompeo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alisema “Tutaendelea kuwa na mazungumzo na mwana mfalme na Saudi Arabia kuhusu hakikisho la uwajibikaji kamili na uliokamilika wenye heshima kwa mauaji yasiyokubalika ya Jamal Khashoggi"

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema Jumapili kwamba Marekani itamueleza mwana mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman kuhakikisha watu ambao walimuuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Tutaendelea kuwa na mazungumzo na mwana mfalme na Saudi Arabia kuhusu hakikisho la uwajibikaji kamili na uliokamilika wenye heshima kwa mauaji yasiyokubalika ya Jamal Khashoggi, Pompeo alisema baada ya mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Khashoggi aliuwawa wakati alipotembelea ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul huko Uturuki mwezi Oktoba mwaka jana. Awali Saudi Arabia ilisema Khashoggi aliondoka ubalozini hapo mwenyewe akiwa salama lakini baadae ubalozi ulikiri aliuwawa ndani ya jengo hilo katika kile maafisa wa Saudi Arabia walichokiita operesheni isiyo salama.

Uturuki ilisema agizo la kumuuwa Khashoggi lilikuja kutoka ngazi za juu za serikali ya Saudi Arabia lakini maafisa wa Saudi Arabia wanaendelea kusema halikuwa agizo kutoka kwa mwana mfalme wa Saudi Arabia.

Pompeo hivi sasa yupo Qatari mji mkuu wa Doha kisha ataelekea Jordan, Iran, Misri, Bahrain na Umoja wa Falme za kiarabu wakati wa ziara yake ya wiki moja mashariki ya kati. Anatarajiwa pia kusafiri kwenda Saudi Arabia.

XS
SM
MD
LG