Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:47

Maseneta : Upo ushahidi Prince Mohammed bin Salman alihusika na mauaji ya Khashoggi


Jamal Khashoggi
Jamal Khashoggi

Maseneta maarufu wa Marekani wamesema Jumanne kuna ushahidi wa kutosha kuwa Prince wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman alihusika na mauaji ya mwandishi mpinzani wa Saudi Arabia ndani ya ubalozi mdogo wa Riyadh mjini Istanbul, wakikataa madai ya Rais Donald Trump kuwa kesi dhidi ya Salman ilikuwa haina ushawishi.

“Iwapo Prince aliyeko madarakani akienda mbele ya washauri wa mahakama, atakutikana na makosa (ya kuuwa) katika muda wa dakika 30,” Seneta Bob Corker, Mwenyekiti wa kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Mambo ya Nje ambaye ni Mrepublikan, amewaambia waandishi wa habari baada ya kusikia taarifa ya mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) Gina Haspel akieleza ushahidi uliokusanywa na wachunguzi wa Marekani juu ya kuuwawa na kukatwakatwa kwa mwili wa Jamal Khashoggi Octoba 2.

Corker amesema “ itakuwa rahisi sana kwa rais kujitokeza” na kusema kuwa Prince “ alimuuwa mwandishi wa habari.” Badala yake, Corker amesema, Trump “anasema ni sawa kufanya hivyo.”

Mbunge mwengine maarufu wa Chama cha Republikan, Seneta Lindsey Graham wa South Carolina, amesema, “ Hakuna ukungu wa moshi wa uhalifu huo, kuna ukungu wa moshi wa msumeno,” akiwa anakusudia matumizi ya msumeno yaliyo fanywa na majasusi wa Saudia katika kuukata kata mwili wa Khashoggi aliyekuwa na umri wa miaka 59.

Mwandishi huyo wa habari alikuwa anaishi Marekani na kuandika makala za maoni katika gazeti la The Washington Post ambazo zilikuwa zinamkosoa Prince Mohammed na Riyadh kujihusisha na vita vya miaka mingi vya Yemen.

Khashoggi alikuwa amekwenda kuchukua makaratasi yake aliokuwa anayahitaji kwa ajili ya kufunga ndoa na mchumba wake Mturuki.

Graham alisema kuwa Prince huyo aliyeko madarakani Saudia ni “mpuuzi,” “Biashara kama kawaida (juu ya kutolewa kwa msaada wa Marekani kwa Saudi Arabia) umefikia kikomo kwa upande wake.

Graham amesema alipewa maelezo na Haspel “akiamini kuwa haiwezekani kabisa” mauaji ya Khashoggi kufanyika bila ya Prince kuwa na taarifa.

Aliondoka katika mkutano huo akiwa na “imani kubwa” kuwa tathmini iliyotolewa ni “sahihi.”

XS
SM
MD
LG