Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 14:13

Ubelgiji yaiomba rasmi msamaha DRC kutokana na vitendo vya utekaji


Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel ameiomba radhi rasmi radhi Ijumaa kutokana na vitendo vya nchi yake kuwateka nyara watoto wa kichotara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kati ya mwaka 1959 na 1962.

Akizungumza mbele ya Baraza Kuu la Bunge Michel alisema nchi yake itafanya juhudi zote katika kupambana na ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni

Watoto hao waliotekwa nyara ni wale waliozaliwa na wazazi wa kizungu na wa Kiafrika kati ya miaka 1940 na 50.

Watoto hao walichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa mama zao wa Kikongo na kupelekwa Ubelgiji ambako walilelewa na familia mbali mbali pamoja na kanisa la Kikatholiki.

Kundi la waathiriwa 25 walihudhuria hotuba hiyo na mwishowe kubaki kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wale waliopoteza maisha wakati wa ukatili huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa ubelgiji kuomba radhi na kukiri kuwajibika kwake kwa ukatili uliotendwa katika miaka 80 ya utawala wake wa kikoloni nchini Congo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG