Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 22:52

CENI -DRC yasema matokeo ya uchaguzi bado hayaja kamilika


Corneille Nangaa
Corneille Nangaa

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamesema Jumapili wanachelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais mpaka baadae wiki hii.

Tume huru ya uchaguzi inafanya mkutano Jumapili kujadili kuchelewesha kutoa matokeo hayo., (huku kukiwa ongezeko la mbinyo kutoka mataifa yenye nguvu na kanisa Katoliki kuheshimu matakwa ya wapiga kura.)

Corneille Nangaa, mkuu wa tume ya uchaguzi (CENI), amesema, "Haitawezekana kutangaza matokeo siku ya Jumapili. Tunapiga hatua lakini hatuna kila kitu bado.”

Nangaa amesema tume mpaka sasa imepokea asilimia 47 ya kura kutoka vituo vya kupigia kura nchini kote nchi kubwa huko Afrika ya Kati, ambayo haina miundombinu.

Kwa upande wao Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini Congo , CENi, lilisema linamatokeo ya uchaguzi juu ya nani aliyeshinda, lakini halikuweza kumtaja mshindi huyo wa uchaguzi wa Congo.

Kiongozi wa ngazi ya juu wa Kanisa Katoliki anataka CENI itowe matokeo ya halali. Kanisa pialimeonya serikali kuwa itakumbwa na hasira za wananchi iwapo matokeo hayo hayatakuwa ya "kweli kwa mujibu wa kura zilizopigwa katika visanduku vya kupigia kura."

XS
SM
MD
LG