Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:15

AU, SADC zasema uchaguzi DRC ulikuwa wa amani


Viongozi wa SADC
Viongozi wa SADC

Umoja wa Afrika umesema katika taarifa yake Jumatano uchaguzi uliofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) 2018, ambapo pia wabunge wa taifa na majimbo walipigiwa kura ulifanyika kwa amani.

Hata hivyo wamekiri kuwa kulikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa vifaa vya kupigia kura.

"Kufanyika kwa uchaguzi huu ni ushindi mkubwa kwa watu wa DRC," umesema ujumbe huo.

"Ujumbe wetu unaamini kwamba matokeo ya uchaguzi yatakuwa yanakwenda sambasamba na matakwa ya wapiga kura."

SADC yapongeza uchaguzi DRC

Wakati huo huo Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imesema Jumatano uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ulikwenda vizuri kwa kiasi fulani pamoja na kuwepo matukio mbalimbali ya vurugu ambayo yalisababisha baadhi ya watu kushindwa kupiga kura.

Tamko hilo la jumuiya ya SADC unakinzana na madai ya wagombea wa upinzani kwamba uchaguzi huo wa Disemba 30 uligubikwa na kasoro kadhaa na kauli ya mbunge mwandamizi wa Marekani kwamba uchaguzi huo "ulikuwa siyo huru na haki."

Angola na Afrika Kusini niwashiriki muhimu wa DRC kwa miaka kadhaa, lakini uhusiano uliingia doa kwa kukataa kwake kuachia madaraka baada ya kumalizika rasmi kwa muhula wake mwaka 2016.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa kauli ya kuwa uchaguzi ulikwenda vizuri iliyotolewa na SADC ni muhimu kwa uhalali wa utawala wa rais yeyote ajakaye shinda nchini DRC.

"Pamoja na changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi, waangalizi wetu wamethibitisha kuwa uchaguzi kwa kiasi fulani ulisimamiwa vizuri," ujumbe wa SADC ulieleza katika taarifa yake.

Uchaguzi uliruhusu "Wakongo walio wengi kutimiza haki yao ya kupiga kura."

Taarifa hiyo ilieleza pia kuwa asilimia 59 ya maeneo ya kupigia kura walioshuhudia yalifunguliwa kwa wakati, shughuli ya kuhesabu kura zilifanyika kwa uwazi na askari polisi waliokuwa wanalinda uchaguzi huo walifanya kazi yao kwa weledi.

Waangalizi wa SADC wamesema wengi wa wapiga kura walitekeleza haki yao ya kikatiba.

XS
SM
MD
LG