Taarifa zinasema dereva wa lori hilo ambaye ni raia wa Tanzania amekamatwa na kuwekwa rumande ikidaiwa kwamba alikuwa amelewa wakati akiendesha lori hilo.
Ajali hiyo ilikuwa baina ya lori iliyokuwa imebeba tindikali ilioligonga basi la abiriya liliokuwa limesimama kituoni, wamesema viongozi wa Wizara ya Afya nchini humo.
Lakini shirika moja la kiraia lililoongea na mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Lubumbashi, nakumfahamisha kuwa watu 30 ndio waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Ripoti zaidi zinasema lori hilo ambalo lilikuwa linasafirisha tindikali kwenda kwenye mgodi unaozalisha madini aina ya Cobalt kwenye mji wa Kolowezi, lilikuwa linatembea kwa mwendo wa kasi.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Patrick Nduwimana, Washington, DC.