Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 15:37

Watu 50 wapoteza maisha ajali ya boti DRC


Ramani ya DRC

Afisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema Ijumaa watu 50 wamepoteza maisha katika ajali ya boti katika mkoa wa kaskazini wa nchi hiyo.

Richard Mboyo Iluke, makamu gavana wa jimbo la Tshuapa, ameliambia shirika la habari la AFP: Tumeweza kuwapata watu 49 Jumatano na mwengine asubuhi ya leo.

Makamu gavana mwengine ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa idadi kama hiyo ya watu ilinusurika katika ajali hiyo.

Ajali zenye kuuwa za boti ni za kawaida nchini DRC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG