Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 21:15

Takwimu za ajali za barabarani Afrika Mashariki 2016


Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza majeraha yanayotokana na ajli za barabarani ni sababu kuu ya vifo na ulemavu kwa watu duniani.

Kulingana na utafiti wake wa mwaka 2016 kwa wastani watu watatu kati ya kila watu elfu 10 hupoteza maisha katika nchi hizo.

Uganda inaongoza ikiwa na idadi kubwa zaidi ya wanaokufa kutokana na ajali hizo, ikifuatiwa na Tanzania, Rwanda, Kenya, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusu ajali hizo kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini Tanzania, Fortunatus Muslim, amesema ajali zimepungua kufikia asilimia 42 kati ya mwaka 2016 na mwaka 2017.

Kwa upande wa Kenya, kwa mujibu wa mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani (NTSA), idadi ya vifo vya madereva imepungua kutoka 177 mwaka 2016 kufikia 149 kwa mwaka 2017, na kwa upande wa abiria na wanaotembea kwa miguu idadi iko karibuni sawa na hiyo.

WHO linaripoti kuwa kati ya watu elfu hadi elfu 13 hupoteza maisha kila mwaka, na wengi ni wale wanaotembea kwa miguu au pikipiki.

Kadhalika WHO inaeleza kwamba Kenya ni moja kati ya mataifa 10 duniani ambako mradi maalum wa usalama barabarani utafanyika kwa kipindi cha miaka mitano.

Mradi huo utahamasisha kuvaa kofia unapoendesha pikipiki, kuendesha gari bila ya kutumia ulevi pamoja na kuelimisha raia juu ya usalama barabarani na polisi kutekeleza sheria za kuweza kupunguza ajali.

Kwa Uganda idadi ya ajli ni ndogo zaidi kuliko Tanzania na Kenya, lakini kufuatana na idadi ya wakazi wake inakuwa mojawapo ya nchi zenye kiwango cha juu cha vifo kutokana na ajali za barabarani.

Kuna wastani wa vifo 29 kwa watu laki moja ukilinganisha wastani wa watu 24 kwa kila watu laki moja barani Afrika kulingana na utafiti wa umoja wa mataifa . Naibu mkurugenzi wa usalama barabarani inspekta wa polisi Dkt Kassin Steven anasema kutokana na hali hiyo juhudi zimechukuliwa kupunguza idadi ya vifo na ajali barabarani.

"Kwa miaka mitano iliyopita tumeweza kupunguza idadi ya vifo barabarani ingawa inabidi kutaja kwamba idadi iliongezeka mwaka jana baada ya kupunguza vifo kutoka elfu 3 hadi elfu 2500 . Hata hivyo kwa mwaka 2017 tunaona vifo vimepungua ukilinganisha na watu elfu 3300 waliofariki mwaka jana."

Dkt Steven anasema juhudi zinaendelea katika kupunguza ajali hizo na ufanisi utatokana na utekelezaji wa sheria.

"Moja ni kuimarisha utekelezaji wa sheria za barabarani katika barabara kuu ambako ajali zinatokea kwa wingi. Pili kuwapokonya madereva leseni zilizopatikana kwa njia zisizo halali, na madereva hao wanachangia sana katika ajali. Na tumeungana na wadau wengine kama vyombo vya habari kuwaelimisha waendeshaji magari juu ya usalama wa barabarani."

Rwanda nayo ilikuwa mojawapo ya nchi zenye ajali mbaya Afrika miaka 10 iliyopita na kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia (WB) idadi imepungua. lakini bado ajali ziko juu ikilinganishwa na nchi za Afrika Mashariki, ambayo ni ya tatu. Ripoti hiyo inaeleza kwamba ajali nyingi zinatokea katika miji mikubwa hasa Kigali. Na kwa mujibu wa takwimu za WHO mwaka 2014, idadi ya vifo ilifikia 2172. Kwa upande wa Burundi katika kipindi kama hicho kulitokea vifo 1,837.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:58 0:00

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG