Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 01, 2023 Local time: 16:42

Mchakato wa kuapishwa Tshisekedi wakosolewa


Rais mpya wa DRC, Felix Tshisekedi

Mchakato uliopelekea kuapishwa kwa Tshisekedi umekosolewa na watu na taasisi mbalimbali kufuatia kile kilichoonekena kama mwingilio wa kisiasa hususan katika uamuzi wa mahakama ya kikatiba iliayosema kwamba Tshisekedi ndiye aliyeshinda uchaguzi wa Desemba 30.

Tume ya uchaguzi ya DRC, CENI, imeshutumiwa na wadau mbalimbali kwamba ilimpokonya ushindi kiongozi mwingine wa upoinzani, Martin Fayulu, licha ya kwamba "alikuwa amepata ushindi mkubwa."

Tayari Fayulu amewataka wafuasi wake kufanya maandamano kupinga kutangazwa kwa Tshisekedi kama rais.

Rais anayeondoka, Joseph Kabila, Jumatano aliwataka Wakongomani kumuunga mkono kiongozi mpya.

Hafla hiyo ya Alhamisi ilihudhuriwa na raia wa Kenya, Uhuru Kenyatta kati ya wageni wengine mashuhuri.

Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti Alhamisi kwamba viongozi wengi wa nchi na seikali waliokuwa wamealikwa hawakuhudhuria sherehe hiyo ya uapisho.

Felix Tshisekedi ni mwanaye mwanasiasa maarufu wa upinzani, marehemu Etiene Tshisekedi.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa kisiasa nchini humo kukabidhiana mamlaka kwa amani katika kipindi cha miaka 60.

Katika hotuba yake, Kiongozi huyo alisema kuwa atahakikisha nchi hiyo haigawanyiki kwa misingi ya chuki na ukabila, na kumpongeza mpinzani wake wa karibu, Martin Fayulu.

"Nampongeza Martin Fayulu kwani ni askari shupavu wa wananchi," alisema Tshisekedi.

Tshisekedi alichukua hatamu za uongozi kutoka kwa Rais Joseph Kabila.

Majaji wa mahakama ya kikatiba DRC
Majaji wa mahakama ya kikatiba DRC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG