Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 01:58

Ushirika wa chama tawala DRC umeshinda viti vingi bungeni


Rais Joseph Kabila wa DRC

Matokeo hayo yatapunguza uwezo wa Tshisekedi kutekeleza ahadi zake za kampeni na kuvunja miaka 18 ya enzi za Kabila na kuzusha khofu kwamba ushindi wake uliotangazwa Alhamis ni wa kupanga

Ushirika wa chama tawala cha Rais wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo-DRC anayeondoka madarakani Joseph Kabila umeshinda viti vingi bungeni katika uchaguzi wa Disemba 30 mwaka jana ofisa mmoja wa ushirika alieleza Jumamosi licha ya ushindi wa kiongozi wa upinzani Felix Tshisekedi katika kura ya urais iliyofanyika siku hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters matokeo hayo yatapunguza uwezo wa Tshisekedi kutekeleza ahadi zake za kampeni na kuvunja miaka 18 ya enzi za Kabila na kuzusha khofu kwamba ushindi wake uliotangazwa Alhamis ni wa kupanga ambapo utahifadhi ushawishi wa Kabila kwenye wizara muhimu na vikosi vya usalama.

Rais Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani katika siku chache zijazo katika kile kinachoelezewa kuwa makabidhiano ya kwanza ya madaraka nchini Congo kwa njia ya demokrasia tangu nchi hiyo ipate uhuru.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG