Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:28

Afrika Kusini, Zambia waishauri CENI kutangaza matokeo DRC


Rais Edgar Lungu
Rais Edgar Lungu

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa Zambia Edgar Lungu wamekutana Jumatano na kutoa tamko la kuishauri tume ya uchaguzi (CENI) nchini Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo (DRC) kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa haraka ili kuendeleza utulivu nchini humo.

Wiki iliyopita, Afrika Kusini, ambaye ni mshirika mkuu wa Kabila, waliungana na Russia na China huko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kuzuia tamko lilopendekezwa na Ufaransa ambalo lilikuwa linapongeza kufanyika uchaguzi lakini likakosoa uamuzi wa serikali kuzima mitandao ya intaneti na mitandao mengine ya jamii.

Tume imetangaza Jumanne jioni kwamba imeanzisha “mikutano kadhaa ya kutathmini na kujadili, na kuwa itapelekea kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais.”

Chanzo cha habari ndani ya tume ya uchaguzi na mwanadiplomasia wamesema wanategemea matokeo kutangazwa baadae Jumatano.

Mwanadiplomasia mwengine, hata hivyo amesema kuwa majumuisho ya kura zote bado hayajakamilika na kuwa kutangazwa kwa matokeo hayo kunaweza kusubirishwa hadi Alhamisi.

Wakati huohuo Askari wa kuzuia fujo wamepelekwa katika makao makuu ya tume ya uchaguzi Kinshasa, Jumatano, wakati kukiwa na wasiwasi juu ya matokeo yenye utata ya uchaguzi wa rais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, uchaguzi ambao tayari umetiwa dosari kwa tuhuma za wizi wa kura.

Majumuisho ya matokeo yanaweza kutangazwa baadae Jumatano baada ya CENI kukutana usiku kucha hadi asubuhi.

Polisi pia wameendelea kulinda doria katika barabara kubwa ya jiji hilo la Kinshasa, wakati wananchi wa Congo wakiwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani wakati kuna hisia ya kuwa serikali ya Rais Joseph Kabila inafaya mazungumzo juu ya makubaliano ya kuwa na serikali ya mseto na kiongozi mmoja wa upinzani.

Uchaguzi wa Disemba 30 ulikusudia kuleta kwa mara ya kwanza kubadilishana kwa madaraka kwa njia ya kidemokrasia kwa nchi hiyo kubwa iliyoko Afrika ya Kati katika kipindi cha miaka 59 ya uhuru wake.

Lakini matokeo yenye utata yanaweza kuibua uvunjifu wa amani ambao uliwahi kutokea baada ya uchaguzi wa 2006 na 2011 na kuivuruga mipaka ya upande wa mashariki ya Congo ambayo tayari haina amani.

XS
SM
MD
LG