Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:48

Trump asema Marekani imejitayarisha baada ya kifo cha kwanza kutangazwa nchini


Rais Donald Trump akizungumza na vyombo vya habari juu ya hali ya kirusi cha corona White House, Feb. 29, 2020, in Washington.
Rais Donald Trump akizungumza na vyombo vya habari juu ya hali ya kirusi cha corona White House, Feb. 29, 2020, in Washington.

Rais wa Marekani Donald Trump, akiwa na Makamu wa Rais Mike Pence na uongozi wake unaoshughulikia mlipuko wa virusi vya corona, Jumamosi alijaribu kulipa moyo taifa juu ya hatua zinazochukuliwa wakati kifo cha kwanza kinachotokana na ugonjwa huu mpya kutangazwa.

Trump alivitaka vyombo vya habari na wanasiasa “wasifanye chochote kile kitakacho chochea hofu kwa sababu hakuna haja ya kuwepo wasiwasi kabisa.”

“Katika hali yoyote ile, tumejiandaa vyema,” alisema.

Uongozi wa Trump umeweka makatazo zaidi ya kusafiri katika safari zinazohusiana na Iran kwa kuwa kunamlipuko mkubwa wa kirusi cha corona huko na tahadhari ya “katazo la kutosafiri” kuelekea maeneo ya Itali na Korea Kusini ambayo yameathiriwa zaidi na kirusi COVID- 19.

Trump amepitisha katazo la raia wa kigeni ambao walisafiri kuelekea Iran katika siku 14 zilizopita, lililotolewa na Pence, ambaye aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inashirikiana na serikali za Itali na Korea Kusinikuimarisha upimaji wa kirusi hicho katika nchi hizo ambao wanasafiri kurejea Marekani.

Makatazo zaidi ya kusafiri huendea yakatolewa, ikiwemo safari kupitia mpaka kati ya Marekani na Mexico.

“Tunatafakari juu ya mipaka yote,” Trump alisema.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG