Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 19:52

China : Wanafunzi wa Kiafrika waeleza hofu ya maambukizo ya kirusi corona


Madaktari wakiwa na mavazi ya kujikinga wakimtibu mgonjwa mwenye homa ya mapafu iliyosabibishwa na kirusi corona katika hospitali ya Zhongnan ya Chuo Kikuu cha Wuhan
Madaktari wakiwa na mavazi ya kujikinga wakimtibu mgonjwa mwenye homa ya mapafu iliyosabibishwa na kirusi corona katika hospitali ya Zhongnan ya Chuo Kikuu cha Wuhan

Wanafunzi kutoka Kenya na Tanzania wameeleza kuwa mlipuko wa kirusi corona nchini China unaendelea kuleta hali ya wasiwasi kutokana na kukosekana kwa tiba kamili ya uhakika.

Mtanzania

Mwanafunzi Jaffari Rajabu anayesomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Tongji Medical University, Hust, Wuhan, China, ameleeza hali hiyo ya wasiwasi katika mahojiano na Sauti ya Amerika (VOA) Jumanne.

Amesema wako wanafunzi 420 kutoka Tanzania ambao wanasoma katika vyuo mbalimbali katika mji wa Wuhan.

Mkenya

Hali hiyo ya wasiwasi pia imeelezwa na mwanafunzi wa uzamivu Anthony Waigwa wa Chuo Kikuu cha Chinese Academy, huko Wuhan.

Anasema wanafunzi wenzake 30 kutoka Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki wana wasiwasi mkubwa wa kupata maambukizo.

Hakuna maambukizo kwa wanafunzi wa Afrika

"Mpaka sasa wanafunzi kutoka Tanzania, Kenya, Ethiopia, Nigeria na Misri wote katika mji huo wa Wuhan na miji mingine hawajapata maambukizo yoyote," amesema Rajabu.

Naye Waigwa amesema wanafunzi wengine wa kigeni kutoka nchi za Afrika na nyingine katika chuo chao mpaka sasa hawajapata maambukizo ya ugonjwa huo.

Wanafunzi hao waliohojiwa na VOA wamesema kuna mawasiliano ya karibu kati ya uongozi wa wanafunzi na ubalozi wa nchi zao.

“Madaktari wanajitahidi kutibu dalili za ugonjwa huo ambazo zinajitokeza kwa wagonjwa hao,” amesema Rajabu.

“Wagonjwa wanaokwenda hospitali wakiwa na dalili za awali wanapatiwa tiba na wanapona, lakini wagonjwa ambao tayari wanaugua wakiwa katika hali mbaya kwa kweli ni kazi kuwahakikishia afya zao,” ameongeza.

Wanafunzi wafuata muongozo wa madaktari

Kwa mujibu wa wanafunzi hao wanafunzi wote wanapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa madaktari, wataalamu wa afya na kutoka ofisi ya jumuiya ya wanafunzi wa kimataifa.

Pamoja na mambo mengine Rajabu amesema wametakiwa wasitoke nje, waepuke msongamano, wavae vitambaa vya kujikinga usoni, waoshe mikono, wawe makini na vyakula. Pia anaeleza kuwa wameshauriwa kutumia dawa mbalimbali ambazo zinaongeza kinga mwilini ikiwemo vitamin c.

“Mahitaji yetu yote ikiwemo chakula yanapelekwa katika maduka ya Supermarket ambako tunatakiwa tukavichukuwe na kuvihifadhi vyumbani mwetu,” amefafanua.

Shughuli zote za uzalishaji zimesimama Wuhan

Akieleza hali ya mji wa Wuhan, Rajabu amesema kuwa shughuli za kila siku zimepungua sana na usafiri wa umma umesitishwa.

“Shughuli za ujenzi, uzalishaji mali zimesimama. Huduma muhimu kama vile hospitali, polisi kudhitibiti watu wasisongamane, magari ya kufanya usafi, maduka ya madawa na maduka ya kuuza chakula zinaendelea.

Kuhusu kuondoka wanafunzi hao nchini China, Rajabu ameeleza kuwa balozi za nchi mbalimbali za Kiafrika zinaendelea kushauriana na serikali ya China na hali ikiwa haidhibitiki anafikiri wataruhusu suala la kuwaondoawanafunzi kutoka eneo hilo.

Ameongeza kuwa ubalozi umewapa tahadhari jinsi ya kujikinga na kutushauri tufuate muongozo uliotolewa na “hatua nyingine ikiwepo kuondolewa ikifikwa watatufahamisha.”

XS
SM
MD
LG