Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:57

Kirusi Corona : Raia wa kigeni waanza kuondoka China baada ya kupimwa


Ndege ya kukodiwa iliyo wasafirisha raia wa Japan kutoka mjini Wuhan baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda, Tokyo Jumatano, Januari 29, 2020. (AP Photo/Eugene Hoshiko)
Ndege ya kukodiwa iliyo wasafirisha raia wa Japan kutoka mjini Wuhan baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda, Tokyo Jumatano, Januari 29, 2020. (AP Photo/Eugene Hoshiko)

Ndege iliyokodiwa iliwasafirisha raia wa Japani 206 kutoka Wuhan, ambayo ndio chimbuko la kirusi hicho, kuelekea uwanja wa ndege wa Haneda, Tokoyo Jumatano.

Abiria wanne walipelekwa hospitali baada ya kusema wanahisi wanaumwa. Wafanyakazi wa afya walikuwa ndani ya ndege ili kuwapima abiria hao kabla ya ndege kuondoka na pia baada ya ndege kutua.

Wamarekani waondolewa Wuhan

Shirika la habari la Associated Press limesema kuwa ndege ya kukodiwa iliwasafirisha kutoka mjini Wuhan idadi isiyojulikana ya Wamarekani hadi mji wa Anchorage, Alaska ambako watapiwa kuangalia iwapo wana kirusi.

Australia, New Zealand, Ufaransa, Urusi na mataifa mengine pia yametangaza mipango ya kuwaondoa raia wake kutoka mjini Wuhan wiki hii.

Pamoja na kuongezeka idadi ya vifo, idara ya afya ya China inasema idadi ya waliothibitishwa kuambukizwa kirusi corona wamefikia 5,900, ikiwa ni idadi kubwa kupita ile ya wale waliokuwa wameambukizwa kirusi cha homa ya mafua, SARS, iliyouwa watu 800 dunia nzima kati ya mwaka 2002 – 2003.

Karantini yawekwa mji wa Wuhan

Serikali imeweka karantini katika mji wa Wuhan, ikizuia watu kuingia na kutoka nje ya mji huo.

Miji mingine kadhaa katika jimbo la Hubei, ambapo Wuhan ni mji mkuu, wanakabiliwa na katazo kali la kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyengine.

Wuhan iko mbioni kukamilisha maeneo mapya mawili ya muda yatakayotumika kutibu idadi ya wagonjwa inayoongezeka. Kirusi hicho kinaaminika kuwa kiliibuka mwishoni mwa mwaka 2019 katika soko la vyakula vya baharini yaliyokuwa yanauza wanyama pori kinyume cha sharia.

UAE yathibitisha maambukizo ya raia wake

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umethibitisha kuwa familia moja ambayo ilikuwa imerejea hivi karibuni kutoka Wuhan imekutikana na kirusi korona na kuwa ni ambukizo la kwanza katika Masharikii ya Kati.

UAE hivi sasa ipo katika orodha ya darzeni za nchi zilizothibitishwa kuwa na kirusi hicho, ikiwemo Australia, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Korea Kusini, Thailand, Marekani na Vietnam.

Shirika la Afya Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema wengi kati ya watu waliokutikana na kirusi corona walikuwa wanahistoria ya kusafiri kwenda Wuhan, na wengine kadhaa walikuwa wamekaribiana na mtu aliyekuwa amesafiri huko.

Tahadhari ya CDC

Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC) ya Marekani (U.S) kimetahadharisha kuwa safari zote zisizo za dharura kwenda China zisitishwe, wakati shirika la ndege la Uingereza limetangaza Jumatano kuwa limesitisha ndege za moja kwa moja kwenda na kutoka China bara.

XS
SM
MD
LG