Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 15:58

Kirusi Corona : Idadi ya walioambukizwa Marekani yafikia watatu


Wasafiri katika treni wakiwa wamevaa vitambaa maalum kwa ajili ya kujihami kupata maambukizi ya kirusi corona, Hong Kong, Januari 25, 2020.
Wasafiri katika treni wakiwa wamevaa vitambaa maalum kwa ajili ya kujihami kupata maambukizi ya kirusi corona, Hong Kong, Januari 25, 2020.

Mgonjwa wa tatu aliyegundulika kuwa na aina mpya ya kirusi kama cha homa ya mapafu kutoka China yuko Kusini mwa California nchini Marekani, maafisa wa afya wamesema.

Kituo cha kudhibiti magonjwa, CDC, kimethibitisha kuwa msafiri kutoka mji wa China, Wuhan – ambako ndio chimbuko la mlipuko wa kirusi hicho – alikutikana na kirusi, Idara ya Afya ya Orange County imetangaza kabla ya saa sita usiku Jumamosi.

Mgonjwa huyo ametengwa katika hospitali mmoja na hali yake inaendelea vizuri, tamko la idara hiyo limesema.

Kirusi hicho kinaweza kusababisha homa, kukohowa, kupumua kwa shida na homa ya mapafu. Kirusi hicho ni sehemu ya familia ya kirusi corona ambacho kinauhusiano na virusi vya SARS na MERS ambavyo vilisababisha milipuko siku za nyuma.

Mgonjwa wa kwanza kupatikana California amegunduliwa baada ya kukutikana na kirusi wagonjwa katika jimbo la Washington, Januari 21 na Chicago, Januari 24. Wagonjwa wote wawili - Washington, mmoja mwanaume, 30, na Chicago, mwanamke, 60, pia walikuwa wamesafiri kwenda China.

Idadi ya waliokufa kutokana na kirusi hicho imefikia 56 nchini China. China imetoa makatazo kadhaa ya kusafiri katika maeneo yaliyoathiriwa vibaya sana katika nchi hiyo ili kuzuia kuenea kwa kirusi hicho.

Kadhalika Ubalozi mdogo wa Marekani huko Wuhan umetangaza Jumapili kuwa utawaondoa wafanyakazi wake na baadhi ya raia wake kwa kutumia ndege ya kukodishwa.

CDC inategemea kuwa Wamarekani zaidi wakutikana na kirusi hicho kipya kilichogunduliwa, ambacho inaaminika kuwa inachukuwa kipindi cha wiki mbili kuweza kujitokeza, wakati idadi ya maambukizo duniani imethibitishwa kukaribia wagonjwa 2,000.

CDC inawapima wasafiri wanaowasili kutoka Wuhan na ndege na wale wanaounganisha ndege zao kupitia Wuhan. Vipimo hivyo vinafanyika katika uwanja wa ndege wa Atlanta, Chicago, New York, San Francisco na Los Angeles.

Muongozo kutoka CDC unashauri kuwa watu ambao walikuwa wamekaribiana katika harakati za kawaida na wagonjwa wenye kirusi “hatari ni ndogo” ya kupata maambukizo.

XS
SM
MD
LG