Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:48

Serikali DRC : Marufuku kuwaficha wagonjwa wa Ebola


Wafanyakazi wa afya wakinyunyiza nyumba dawa katika kitongoji cha Tchomia, eneo lililokuwa na mlipuko wa Ebola mashariki mwa DRC, Septemba 27, 2018.
Wafanyakazi wa afya wakinyunyiza nyumba dawa katika kitongoji cha Tchomia, eneo lililokuwa na mlipuko wa Ebola mashariki mwa DRC, Septemba 27, 2018.

Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imepiga marufuku kitendo cha kuwaficha wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola na kuahidi watahakikisha polisi wanatoa ulinzi wa kutosha kwa maafisa wa afya wanaofanya shughuli za mazishi.

Hatua hiyo inalenga kukabiliana na ongezeko la maambukizo ya Ebola nchini humo na kushambuliwa kwa maafisa wa afya..

Vyanzo vya habari vinasema kuwa wakazi wa eneo la mashariki mwa DRC wamewashambulia maafisa wa afya na kukataa kushirikiana na serikali katika juhudi za kupambana na mlipuko wa Ebola ambao inaaminika kuwa umeuwa watu 118 tangu mwezi Julai 2018.

Ebola imesambaa hadi mji wa Beni, wenye maelfu ya watu na kuambukiza watu kadhaa.

Maafisa wanasema kwamba hawawezi kufaulu katika kukabiliana na ugonjwa huo iwapo hakuna ushirikiano kutoka kwa raia, huku kisa kimoja au viwili, vya maambukizi mapya, vikiripotiwa kila siku.

XS
SM
MD
LG