Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 14:07

Ebola : WHO yaikosoa Tanzania kwa kutotoa ushirikiano


Shirika la Afya Duniani (WHO) limeikosoa Tanzania kwa kutotoa ushirikiano juu ya taarifa za uwezekano wa kuwepo matukio ya Ebola nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza, Reuters, WHO imeeleza katika taarifa yake kuwa lilipata taarifa kuna mgonjwa mmoja aliyeshukiwa kuwa na maambukizo hayo aliyefariki Dar es Salaam, na wagonjwa wengine wawili lakini hata baada ya shirika hilo kuomba mara kadhaa taarifa juu ya matukio hayo, halikupewa ushirikiano.

Hata hivyo Tanzania imesema kuwa haina mgonjwa yoyote anayeshukiwa kuwa na Ebola au kuthibitishwa kuwa na virusi.

Katika mlipuko wa hivi karibuni Ebola imeuwa zaidi ya watu 2,000 huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakati Uganda ikiendelea kupambana kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Ugonjwa huo wenye kuambukiza kwa kasi uliathiri baadhi ya maeneo ya Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016 na kuua zaidi ya watu 11,000.

Nini ambacho WHO inakilalamikia?

Tamko lake la Jumapili limesema kuwa Septemba 10, 2019, shirika hilo lilipata taarifa kuwepo kwa mgonjwa anayeshukiwa kuwa na maambukizo mjini Dar es Salaam, mji uliokuwa na watu wengi zaidi Tanzania, katika kile ambacho kinasadikiwa kuwa ni tukio la kwanza la Ebola nchini.

Tamko hilo lilieleza kuwa mgonjwa huyo alikuwa nchini Uganda, akaonekana na dalili za Ebola Agosti, 2019, akapimwa na kuonekana na virusi, alifariki Septemba 8, 2019. Watu waliokutana na mwanamke huyo waliwekewa karantini.

WHO inasema ina taarifa ambazo sio rasmi za uwezekano wa kuwepo wagonjwa wengine wawili.

XS
SM
MD
LG