Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 01:54

UN : Msaada wa dharura wahitajika DRC kukabiliana na Ebola


Mmoja wa walionusurika baada ya kuambukizwa Furana Katungu, miaka 2-year-old akiwa wodini katika kitengo cha dharura Biosecure Emergency Care Unit (CUBE), kituo cha ALIMA, Beni, DRC, Machi 31, 2019
Mmoja wa walionusurika baada ya kuambukizwa Furana Katungu, miaka 2-year-old akiwa wodini katika kitengo cha dharura Biosecure Emergency Care Unit (CUBE), kituo cha ALIMA, Beni, DRC, Machi 31, 2019

Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa kumekuwa na matukio makubwa kadhaa ya uvunjifu wa amani ambayo yameyumbisha juhudi zote za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola huko Butembo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na maeneo ya vituo vya afya yalioko jirani wiki hii.

Kwa mujibu wa msemaji wa UN Farhan Haq wakati operesheni zikiwa zimezinduliwa upya Ijumaa, WHO inamatumaini kwamba harakati za kuchukuwa vipimo katika maabara ambazo bado zinakabiliwa na vizuizi, vitapelekea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wenye virusi vya Ebola katika siku zijazo.

Mlipuko huu uko katika hatua hatarishi, ambako kunaongezeko la maambukizi katika wiki za hivi karibuni jambo ambalo linahatarisha kuenea kwa maambukizi hayo katika majimbo mengine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi jirani.

WHO imesema kunahitajika msukumo mkubwa wa msaada wa kisiasa na kifedha kutoka kwa wahusika nchini DRC na Kimataifa kukabiliana na hali hiyo tata.

Pengo la fedha liliopo hivi sasa linaweza kupelekea WHO na washirika wake kusitisha baadhi ya shughuli ambazo kwa yakini zinahitajika sana.

Hadi Mei 2, WHO ilikuwa tayari imepokea dola za Marekani milioni 32.5 zilizokuwa zinahitajika kuendeleza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo kwa kiwango kilichofikiwa hivi sasa.

Pia wiki hii, kikundi cha ushauri wa chanjo cha WHO kimependekeza muelekeo mpya ambao utawezesha kuwafikia wananchi wengi zaidi na kwa haraka zaidi, hasa ikizingatiwa hali ya ukosefu wa amani inayoendelea na kuweza kupata mrejesho kutoka kwa jamii zilizoathiriwa na ugonjwa huo.

XS
SM
MD
LG