Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 23:57

DRC yajaribu dawa ya kutibu Ebola


Maafisa wa DRC na WHO wakisimamia mpango wa chanjo ya Ebola katika mji wa Mangina, karibu na Beni, Kivu Kivu province, Aug,8, 2018.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza kutumia dawa ya majaribio kutibu wagonjwa wa ebola mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza dawa hiyo kutumika tangu mlipuko wa Ebola mapema mwezi huu.

Maafisa wa afya wa serikali wanasema wameanza kutumia dawa hiyo ya majaribio – inayojulikana kama mAb114 mashariki mwa nchi hiyo ambako ugonjwa wa Ebola ulilipuka mapema mwezi huu katika mkoa wa Beni.

Maafisa pia wamesema kuwa mlipuko huo sasa umeenea katika jimbo jirani la Ituri ambako mtu mmoja amethibitishwa kufa baada ya kurudi nyumbani akitoka Mangina katika jimbo la Kivu Kaskazini ambako ugonjwa huo ulianzia.

Wagonjwa watano wapya wamethibitishwa kulingana na wizara ya afya ya Congo, na kufanya idadi ya wagonjwa kufikia 57. Inakisiwa kuwa watu 41 wamefariki mpaka sasa kutoka na ugonjwa huo,

Dawa ya mAb114 imetengenezwa marekani na taasisi ya afya ya taifa – NIH – kwa kutumia vinasaba vilivyotokana na wagonjwa wa Ebola kutoka mji wa Kikwit – magharibi ya Congo ambako ugonjwa huo ulilipuka mwaka 1995.

Wizara ya afya ya Congo imesema pia kuna aina nyingine ya dawa za majaribio ambazo tayari zimefikishwa Beni zikisubiri kuidhinishwa na kamati za maadali kabla ya kuanza kutumiwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG