Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:41

Kirusi corona : Kifo cha daktari chapelekea maombolezo, hasira dhidi ya maafisa wa China


Picha ya Daktari Li Wenliang kabla ya kupatwa na kirusi na baada yake amethibishwa kufariki Februari 7 katika Hospitali ya Kati ya Wuhan , China.
Picha ya Daktari Li Wenliang kabla ya kupatwa na kirusi na baada yake amethibishwa kufariki Februari 7 katika Hospitali ya Kati ya Wuhan , China.

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa virusi vya corona imeongezeka na kufikia 636 akiwemo Daktari Li Wenliang, aliyekuwa wa kwanza kutahadharisha juu ya ugonjwa huu ambaye alikaripiwa na jeshi la polisi nchini China.

Mlipuko huo hadi sasa umeathiri watu zaidi ya elfu 31,000 kote duniani, ukisababisha marufuku ya safari na watu kuwekwa katika karantini.

Wakati huo huo Rais wa China Xi Jinping amemwambia Rais wa Marekani Donald Trump kwa njia ya simu kwamba ana uhakika kwamba nchi yake itaweza kudhibiti kirusi corona.

Kifo cha daktari Li Wenliang ambaye alikemewa kwa kutahadharisha kirusi kipya kilichoibuka China kulipelekea salamu za pongezi kutumwa kwa wingi kwake Ijumaa na hasira dhidi ya serikali ya kikomunisti kumiminika kwa kutanguliza siasa kuliko usalama wa umma.

Katika kifo hicho, Dr Li Wenliang amekuwa ni sura ya ghadhabu inayotokota katika jamii juu ya Chama cha Kikomunisti kudhibiti taarifa na malalamiko kuwa maafisa wanasema uongo au kuficha milipuko ya magonjwa, kusambaa kwa kemikali, bidhaa hatari zinazouzwa kwa wateja na wizi wa fedha.

Daktari huyo mwenye umri wa miaka 34 amekufa usiku wa Alhamisi katika Hospitali ya Kati ya Wuhan, ambako alifanya kazi na inawezekana ndiko alikopata kirusi wakati akiwatibu wagonjwa siku za awali za mlipuko huo.

Wakati ambapo China na raia wake wanaomboleza na kumtaja kama shujaa daktari aliyekuwa mstari wa mbele kufichua mlipuko wa corona. Dr. Li Wenliang ni miongoni mwa waliokufa.

Daktari huyo alifanya kazi katika kituo cha mlipuko wa ugonjwa huo – Wuhan, alithibitisha kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita kwamba alikuwa na kirusi corona.

Watu wanatoa rambirambi zao katika mitandao na mitaa ya Beijing. Baadhi yao wanasema ameonyesha mfano bora kwenye jumuiya, akiwa mkweli na mwaminifu . vyombo vya habari vya taifa la China ijumaa vimeripoti kwamba uchunguzi utafanywa kufuatia kesi ya Dr. Li.


XS
SM
MD
LG