Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 22:08

China yaomba vifaa vya kuzuia maambukizo ya kirusi corona


Wawekezaji waangalia harakati masoko ya Hisa ya kampuni ya biashara huko Hangzhou, China. Baadhi ya hisa kubwa zilianguka kutokana na mlipuko wa kirusi corona kuendelea kuenea huko China, Februari 3, 2020.

Serikali ya China imetangaza Jumatatu kwamba inahitaji misaada ya vifaa vya huduma za afya na maski zinazotumika katika vyumba vya upasuaji wakati idadi ya vifo kutokana na ugonjwa unaosababishwa na kirusi corona ikiongezeka na kufikia 360.

Idadi hiyo hivi sasa imepita idadi ya vifo vilivyotokea wakati wa mlipuko wa homa ya mafua, Sars, miaka 20 iliyopita, na idadi ya watu walioambukizwa imepinduk 17 200.

Idadi ya vifo 57 vilivoripotiwa Jumatatu ni idadi kubwa ya siku moja tangu ugonjwa kugunduliwa mwaka 2019 katika mji wa kati wa Wuhan.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje Hua Chunying amewaambia waandishi habari kwamba China inahitaji kwa dharura maski na mavazi ya kujikinga na maambukizi ya virusi.

Tangazo hilo limetolewa wakati serikali ya Bejing ilikuwa inafungua hospitali ya muda yenye vitanda elfu 1 iliyojengwa kwa haraka ili kuweza kukabiliana na mlipuko huo wa kirusi corona.

Virusi hivyo vimeshaenea katika nchi 24 za dunia licha ya kwamba serikali mbali mbali zinachukuwa hatua za tahadhari ambazo hazijawahi kushuhudiwa.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Gehebreyesus amesema Jumatatu kwamba hakuna haja ya kuchukua hatua ambazo zitaingilia kati usafiri wa kimataifa na biashara katika kujaribu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Tedros ameiambia bodi ya watendaji wakuu wa WHO kwamba wanatoa wito kwa nchi zote kutekeleza maamuzi kulingana na ushahidi uliyopo, akirudia uamuzi wake wa mwishoni mwa Januari alipotangaza dharura ya kimataifa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG