Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 03:18

Uchaguzi Mkuu Marekani 2016 : Shauku yaongezeka nchini Marekani kujua ripoti ya Mchunguzi Maalum imeibua nini?


Wamarekani wenye shauku ya kujua nini kimejiri katika ripoti ya taifa la nje kuingilia kati kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani 2016 wamelazimishwa kusubiri kidogo zaidi Jumamosi kabla ya muhtasari huo kutolewa rasmi na Idara ya Sheria.

Mueller aliwasilisha ripoti ya siri juu ya uchunguzi wake Ijumaa kwa Mwanasheria Mkuu William Barr, ambaye baadae aliwajulisha viongozi wa bunge la Marekani – Congress kwa njia ya kuwatumia barua kwamba “Kunauwezekano nikawashauri juu ya hitimisho la msingi la mchunguzi maalum katika ripoti hiyo mapema wikiendi hii.

Lakini Barr alitumia siku ya Jumamosi kuipitia ripoti hiyo, na mpaka wakati wa mchana, kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya Sheria, muhtasari wa ripoti hiyo kutoka kwake haukutarajiwa kuifikia Congress pengine hadi siku ya pili.

Msemaji wa White House Hogan Gidley amesema kuwa ofisi yao ilikuwa haijapokea na wala haijapewa muhtasari wowote juu ya ripoti hiyo. Alirudia kusema kile alichosema siku moja kabla mratibu wa vyombo vya habari wa White House Sarah Sanders, kwamba hatua inayofuatia katika uchunguzi huu ni suala linalomhusu Barr.

Swali la msingi la Mueller

Swali la msingi la Mueller, mkurugenzi wa zamani wa FBI, ambalo anatafuta majibu : Ni iwapo Trump na wasaidizi wake walishirikiana na Warusi kuchafua kampeni ya mgombea wa chama cha Demokrat Hillary Clinton, mwaka 2016, kwa kutuma barua pepe zenye kudhalilisha zilizoibiwa kutoka Kamati ya Taifa ya chama cha Demokrat na mwenyekiti wa kampeni ya Clinton? Au iwapo Trump alikuwa amenufaika bila ya kukusudia na mbinu chafu za Russia? Na iwapo rais alijaribu kuharibu uchunguzi uliofuatia ili kujilinda yeye mwenyewe na washauri wa kisiasa na wasaidizi wake?

Huu ndio ujumbe wa Idara ya Sheria kwa bunge la Congress juu ya hitimisho la uchunguzi uliofanywa na Mueller.

Uchunguzi huo umepelekea kukutikana na makosa ya kujibu watu binafsi 37 na vikundi mbalimbali, wengi wao ni majasusi wa Russia ambao hawajakamatwa mpaka sasa. Watu saba, wakiwemo washiriki wa Trump, tayari wamekubali makosa na watano kati yao wamehukumiwa kwenda jela.

Waliokutwa na hatia

Kati yao wenye kesi zilizokuwa na umashuhuri mkubwa, ni mshauri wa usalama wa zamani Michael Flynn aliyekiri makosa yake ya kuidanganya Idara ya upelelezi ya makosa ya jinai (FBI) juu ya mazungumzo yake na balozi wa Russia, na Paul Manafort, mwenyekiti wa zamani wa kampeni ya rais, ambaye hivi karibuni alihukumiwa kwa kutenda makosa kadhaa ya jinai.

Kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo, kulikuwa na hisia zilizoenea kuwa mwendesha mashtaka maalum ataongeza idadi ya wenye kesi za kujibu, lakini hakuna hatua za ziada za kisheria zilizotakiwa kuchukuliwa, kabla ya kutolewa ripoti hiyo kwa Idara ya Sheria.

Wakati ripoti ikiwa imekabidhiwa, uchunguzi wa Mueller ndio umekamilika ipasavyo, lakini sio matatizo ya kisheria ya rais.

Katika miezi ya hivi karibuni, Mueller amepeleka sehemu ya uchunguzi wake katika ofisi za waendesha mashtaka wa Marekani mbalimbali, ikiwemo ofisi ya Wilaya ya Kusini, New York, ambako waendesha mashtaka wamefunguwa uchunguzi wakujitegemea kwa Taasisi ya Trump na biashara nyingine mbalimbali binafsi za Trump.

Mahali kesi ilipofikia?

Iwapo ripoti ya Mueller itapelekea kuwa rais hana makosa, au kupatikana na makosa na kuondolewa madarakani, au kuna mkanganyiko wa aina fulani, kati ya hali hizi mbadala haijulikani nini hatma yake kwa hivi sasa.

Kisheria, Barr ataamua sehemu zipi -iwapo zipo- katika ripoti hiyo kuitoa kwa Bunge la Marekani na kwa umma.

Trump amerejea mara kadhaa kusema kuwa uchunguzi wa mwendesha mshtaka maalum ni “kutafuta mchawi” na anasisitiza kuwa hakuna ushahidi wa kuwa yeye alikula njama na Russia.

Wakati rais amekuwa akisema “sijali “ iwapo ripoti hiyo itatolewa kwa umma, kunauwezekano ikawa kuna mvutano mkubwa wa kisheria kati ya White House, Idara ya Sheria, mawakili binafsi wa Trump na Bunge kabla ya sehemu au ripoti yote kutolewa.

Kanuni za Idara ya Sheria zinamtaka Mueller kukabidhi “ripoti ya siri” juu ya yaliyobainika katika uchunguzi wake kwa mwanasheria mkuu, na mwanasheria mkuu huyo “kulijulisha” Bunge juu ya ripoti hiyo. Hakuna sehemu inayomtaka Mueller kutoa ripoti hiyo kwa umma.

White House

Msemaji wa White House Sarah Sanders amesema katika tamko lake Ijumaa, “ Hatua zinazofuatia ni uamuzi wa Mwanasheria Mkuu Barr, na tunasubiri mchakato huo kuanza kwenda mbele. White House haijapokea au kupewa muhtsari wa ripoti hiyo ya mwendesha mashtaka maalum.”

Kokote ambako ripoti hii itaipeleka Marekani kama nchi, kufahamu wapi ilipoanzia na njia iliyopita itakuwa ni kila kitu hata kidogo kuwa muhimu kama vile kuelewa hatma ya uchunguzi huu.

Mwanzo wa uchunguzi huu

Uchunguzi uliofanywa na mwendesha mashtaka maalum ulianza Mei 17, 2017, baada ya Naibu Mwanasheria Mkuu Rod J. Rosenstein kutangaza kuwa alikuwa amemteua Mueller kuendeleza uchunguzi uliokuwa unaendelea kufanywa na FBI kuangalia mafungamano kati ya kampeni ya Trump na Russia kuingilia kati uchaguzi.

Wakati huo, Rosenstein alisisitiza kuwa kuchaguliwa kwa mwendesha mashtaka maalum kusichukuliwe kama ni uthibitisho kuwa kulikuwa na mawasiliano yeyote kinyume cha sheria kati ya kampeni ya Trump na maafisa wa Russia, na kusema kuwa kukabidhi kwake udhibiti wa siku hadi siku wa uchunguzi huo kwa Mueller ulikusudia kuwahakikishia umma kuwa hauna upendeleo wa kisiasa.

Mueller hakuwa anaanza upya uchunguzi huo. Uchunguzi huo aliokabidhiwa ulikuwa tayari umeanza takriban mwaka mmoja kabla, Julai 31, 2016, baada ya FBI kujua kwamba kunauwezekano kulikuwa makubaliano ya hujma kati ya washauri wa kampeni ya Trump na Russia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG