Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:07

Russia yakanusha shutma za udukuzi


 Dmitry Peskov
Dmitry Peskov

Russia imekanusha kuhusika na udukuzi, siku moja baada ya idara ya sheria ya Marekani kutangaza kuwa itawashtaki majasusi wawili kutoka Russia.

Pia watu wengine wawili wanaoshukiwa kwa wizi wa mamilioni ya nyaraka kutoka kwa mtandao wa Yahoo kufuatia udukuzi uliofanyika mwaka 2014.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amewaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi kuwa hakuna afisi yoyote ya Russia, ikiwa ni pamoja na huduma ya usalama wa kitaifa, FSB, ambayo ilihusika katika vitendo hivyo.

Naibu wa mwanasheria mkuu wa Marekani, Mary McCord, alisema idara hiyo itawafungulia mashtaka maafisa wawili wa FSB na wadukuzi wawili ambao waliwasaidia kwenye uhalifu huo.

XS
SM
MD
LG