Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 02:06

Trump amchagua Barr kuongoza Wizara ya Sheria


William Barr

Mwanasheria Mkuu wa zamani anaye julikana anaunga mkono rais kuwa na madaraka yaliopindukia ni chaguo la Rais Donald Trump kwamba kwa mara nyengine aendeshe Wizara ya Sheria.

Trump amesema Ijumaa kuwa William Barr, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wakati wa utawala wa hayati Rais wa zamani George H.W. Bush ni chaguo lake, akimuelezea kama mtu mwema, na mtu mahiri.

Rais amewaambia waandishi wa habari wakiwa White House kwamba Barr, ambaye ni Mrepublikan, M-Conservative mwenye umri wa miaka 68 na ni wakili wa kampuni, “ alikuwa chaguo langu tangu siku ya kwanza. Anaheshimiwa na Warepublikan na kuheshimiwa na Wademokrat.”

Barr atamrithi kaimu Mwanasheria Mkuu Matthew Whitaker, ambaye aliteuliwa na rais kuongoza Wizara ya Sheria mwezi uliopita baada ya Trump kumfukuza kazi Jeff Sessions, ambaye ni Seneta wa Marekani wa zamani na mmoja wa wale walio muunga mkono Trump hapo awali katika uchaguzi mkuu 2016.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG