Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:26

Trump-Xi wafikia maelewano ya awali Argentina


Rais Donald Trump na Rais wa China Xi Jinping wakati wa mazungumzo yao ya ushirikiano wa nchi hizo mbili katika mkutano wa G-20, Desemba 1, 2018, mjini Buenos Aires, Argentina.
Rais Donald Trump na Rais wa China Xi Jinping wakati wa mazungumzo yao ya ushirikiano wa nchi hizo mbili katika mkutano wa G-20, Desemba 1, 2018, mjini Buenos Aires, Argentina.

Nchi mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani wamekubaliana kufikia masikilizano madogo katika vita iliyokuwa inaongezeka ya kibiashara baada ya kukutana kwa marais Donald Trump na Xi Jinping katika mkutano wa nchi tajiri zenye viwanda G20.

Trump akiongea na waandishi wa habari katika ndege ya rais Air Force One baada ya ndege kuondoka Argentina, amesema makubaliano yaliofikiwa wakati wa chakula cha usiku na Xi, yatakuwa katika historia “kama moja ya makubaliano makubwa yaliyowahi kufikiwa…Na yatakuwa na athari kubwa chanya katika kilimo, bidhaa za viwandani na kompyuta – kila aina ya bidhaa.”

Trump amekubali kuwa ushuru wa bidhaa za China zenye thamani ya dola za Marekani milioni 200 kuendelea kuwa asilimia 10, na hatoongeza ushuru huo hadi asilimia 25, kwa hivi sasa, kama alivyokuwa ametishia kutekeleza hilo ongezeko ifikapo Januari 1, kwa mujibu wa tamko la White House.

Trump na Xi pia “ wamekubaliana mara moja kuanza mazungumzo ya mabadiliko ya miundo ya kuhamisha teknolojia, kulinda haki miliki za kitaaluma, mazungumzo juu ya bidhaa zisizo kuwa na vikwazo vya ushuru, udukuzi wa mitandao na wizi wa kimitandao, huduma na kilimo, kwa mujibu wa tamko la White House.

“Pande zote zimekubaliana kuwa wataendelea kufanya juhudi za kukamilisha majadiliano haya katika kipindi cha siku 90. Na iwapo muda huu utamalizika na pande hizi mbili hazijafikia makubaliano, ushuru huu wa asilimia 10 utaongezeka hadi asilimia 25.

Baadhi ya maelezo hayo yalifafanuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye alithibitisha kuwa nchi zote mbili zitaanza mazungumzo.

Habari hizi bila shaka zitaleta furaha Jumatatu katika masoko ya fedha ya kimataifa, ambazo zimekuwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa vita ya kibiashara kati ya China na Marekani.

XS
SM
MD
LG