Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:07

G20 : Marekani, Canada, Mexico wasaini mkataba mpya wa biashara


Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, kushoto, akipeana mkono na Rais Donald Trump wakati Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akishuhudia wakati wakijiandaa kusaini mkataba mpya wa biashara ukiwa ni mbadala wa mkataba wa NAFTA.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, kushoto, akipeana mkono na Rais Donald Trump wakati Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akishuhudia wakati wakijiandaa kusaini mkataba mpya wa biashara ukiwa ni mbadala wa mkataba wa NAFTA.

Viongozi wa Canada, Mexico na Marekani wamesaini Ijumaa makubaliano mapya ya Amerika Kaskazini.

Justin Trudeau, Enrique Pena Nieto na Donald Trump wanasaini makubaliano hayo huko Argentina kabla ya kufunguliwa mkutano wa nchi za G-20.

Hata hivyo itachukuwa muda kwa mkataba huo kuanza kutumika wakati wabunge wa nchi hizo tatu lazima wapitishe mradi huo, unao julikana kama mkataba wa US-Mexico-Canada, au USMCA.

Mkataba huo unaboresha biashara ya mwaka mzima ya dola za Marekani bilioni 1.2 kati ya nchi hizo tatu.

Inakuwa ni mbadala wa NAFTA, mkataba ambao Trump alikuwa ameukosoa kwa jumla katika kampeni yake ya kinyang’anyiro cha urais cha 2016, akiuita ni mkataba wa kibiashara mbovu kuliko yote katika historia na kuilaumu NAFTA kwa kupotea kwa nafasi za kazi katika viwanda tangu ulipoanza kutumika mwaka 1994.

Wakati nchi hizo tatu zilipokubaliana juu ya mkataba wa USMCA mapema mwaka huu, kiongozi wa Marekani amesema, “ Mkataba huu wa kipekee utaleta fedha na nafasi za kazi nchini Marekani na Amerika ya Kaskazini.

Joshua Meltzer, mtafiti wa ngazi ya juu wa taasisi ya Brookings, ameiambia VOA kuwa wakati ule makubaliano hayo hayakuwa tofauti sana na ya NAFTA.

XS
SM
MD
LG