Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:51

Rais Trump na mkewe watoa heshima zao kwa Bush 41


Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump

Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania walitoa heshima zao Jumatatu jioni mbele ya jeneza la Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush ambaye mwili wake unalala kati kati ya ukumbi mkubwa wa bunge unaofahamika kama Capitol Rotunda na kuwapatia nafasi pia wamarekani kutoa heshima zao kwa Rais wa 41 wa Marekani.

Trump na mkewe walisimama kwa takribani dakika moja kabla ya Rais Trump kumpigia saluti marehemu Bush na kisha Trump aligeuka na kuondoka na mkewe. Jengo la bunge lipo wazi kwa ajili ya waheshimiwa na raia wa kawaida kutoa heshima zao hadi Jumatano.

Wageni pia wanaruhusiwa kutembea kuzunguka uzio wa mahala lilipowekwa jeneza la Bush. Rais huyo wa zamani wa Marekani alifariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 94 akiwa nyumbani kwake kwenye jimbo la Texas nchini Marekani baada ya afya yake kuzorota kwa miaka kadhaa.

Jeneza la Rais huyo wa 41 lilipakiwa kwenye ndege Jumatatu kutoka Texas kwa kupigiwa mizinga 21 na kusafirishwa kwa ndege ya Rais iliyotolewa na Rais Trump hadi kituo cha jeshi la anga cha Andrew kilichopo jimbo la Maryland.

Gari maalum lilibeba jeneza ambalo lilifunikwa kwa bendera ya Marekani na lilienda moja kwa moja hadi kwenye bunge la Marekani mahala ambapo bendi ya jeshi la Marekani ilitoa burudani wakati familia na marafiki walipokusanyika pamoja.

Mtoto wa kiume wa Rais wa zamani wa 41 ambaye pia alikuwa Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush alionekana mwenye huzuni wakati alipoliangalia jeneza la baba yake mzazi lilipowekwa kwenye eneo maalumu kwenye Capitol Rotunda.

XS
SM
MD
LG