Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 21:47

Trump amfukuza kazi Waziri wa Sheria


Rais Donald Trump

Rais Donald Trump wa Marekani amemfukuza kazi waziri wake wa sheria Jeff Sessions baada ya kumtaka awasilishe barua ya kujiuzulu.

Hii imetokea siku moja baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula 2018, ambapo chama cha Republikan kilipoteza udhibiti wake wa Baraza la Wawakilishi.

Sessions amekiri kwa waandishi wa habari kwamba Rais Trump alikuwa amemkasirikia, lakini amesema ilikuwa ni heshima kubwa kwake kuongoza wizara hiyo.

Rais ameonekana siku za nyuma akimkosoa mwanasheria mkuu huyo kutokana na kutoridhika na utendaji wake wa kazi na hasa kitendo chake cha kujiweka pembeni katika uchunguzi unaomkabili rais.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG