Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:25

Trump : 'Namheshimu Rais wa Russia Vladimir Putin, lakini…'


Rais Donald Trump - Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais Donald Trump - Rais wa Russia Vladimir Putin

Rais Donald Trump amesema ijapokuwa “anamheshimu” Rais wa Russia Vladimir Putin sio lazima kuwa mtangamano wao utadumu.

“Lakini nasema ni bora kushirikiana na Russia kuliko vinginevyo. Na kama Russia itatusaidia katika kupambana na kundi la Islamic State, ambayo ni vita kubwa, na ugaidi wa kiislamu dunia nzima—hilo ni jambo zuri,” Trump ameliambia shirika la Televisheni la Fox News katika mahojiano yake ambayo yatatangazwa Jumapili.

“Je nitaweza kushirikiana naye? Sina wazo lolote kuhusu hilo.”

Udhalimu wa Putin

Alipoulizwa kuhusu mauaji alioyafanya Putin siku za nyuma, na jinsi gani Trump angeweza kumheshimu hata baada ya kujua historia yake, Trump ameifananisha Russia na Marekani.

“Kuna wauaji wengi. Sisi pia tunao wauaji wengi. Unafikiria nini? Nchi yetu haina makossa? amesema hayo, kwa mujibu wa sehemu ya maelezo hayo yaliyo patikana kutoka katika mahojiano yake na Fox News siku ya Jumapili.

Kiongozi wa Baraza la Seneti

Mitch McConnell
Mitch McConnell

Akijibu juu ya maoni haya ya Trump kwenye televisheni ya CNN, kiongozi wa wengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell amesema yeye hafikirii “tunaweza kuilinganisha” Marekani na Putin.


Mashirika ya kipelelezi Marekani yameishutumu Russia kwa udukuzi wa kompyuta zilizokuwa zikitumiwa na Chama cha Demokratik kama njama ya kampeni pana za Russia kuvuruga uchaguzi wa urais wa Marekani.

Kabla ya kuchukuwa madaraka, Trump alirejea mara nyingi kudadisi taarifa za jumuiya ya kipelelezi. Lakini ukosoaji wake umesita kwa muda sasa. Bado, rais ameendelea kusema hadharani kwamba yuko tayari kwa mahusiano bora na Moscow.

Mazungumzo ya Trump na Putin

Trump na Rais wa Russia walikuwa katika mazungumzo ya simu siku ya Jumamosi katika kile White House ilichokiita kama “ ni mwanzo muhimu katika kuboresha mahusiano kati ya Marekani na Russia jambo ambalo lilikuwa linahitaji hatua hiyo.”

Vipande ya mahojiano hayo vina swali linalo ongelea agizo la Trump kuhusu uchunguzi wa wizi wa kura katika uchaguzi wa urais Novemba.

Madai dhidi ya Hillary

Hillary Clinton
Hillary Clinton

Trump amedai mara nyingi kuwa wahamiaji haramu walopiga kura wamemzuilia kupata kura ya umaarufu. Trump alishinda kura za wajumbe “Electoral College” lakini alipoteza kura za umaarufu kwa idadi ya kura milioni 2.9 ambazo zilichukuliwa na mgombea wa Demokratik Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu mwaka jana.

“Nataka niwaambie unapoona wahamiaji haramu – watu ambao sio raia na wapo katika usajili wa kupiga kura,” Trump amesema. “Utawaona wahamiaji haramu, wako watu waliokwisha kufa, una haya yote, ni hali mbaya sana, kwa kweli ni mbaya.”

Hata hivyo maafisa wa uchaguzi ambao walizichambua kura za Novemba 8 wanasema hakukuwa na dalili yeyote ya wizi wa kura, kwa kweli sio katika kiwango kinachoelezewa na Trump.

XS
SM
MD
LG