Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 17:01

Mshauri wa Trump akamatwa kujibu mashtaka ya kuvuruga ushahidi, kuzuia sheria


Roger Stone
Roger Stone

Roger Stone, mshauri wa kampeni ya uchaguzi wa Rais Donald Trump, amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya makosa kadhaa ya jinai yanayo tokana na uchunguzi unaofanywa na mchunguzi maalum juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016.

Maafisa wa vyombo vya usalama serikali kuu walimkamata Stone mapema siku ya Ijumaa upande wa kusini mashariki mwa Florida baada ya washauri wa mahakama ya serikali kuu kusema kuwa ana kesi ya kujibu juu ya mambo matano ya kutoa matamko ya uongo na kila moja katika hayo ni la kuzuia uchunguzi na kuwashawishi mashahidi kusema uongo.

Stone ataletwa katika mahakama ya serikali kuu huko Fort Lauderdale, Florida, baadae siku ya Ijumaa, ofisi ya Mueller imeeleza.

Stone alikuwa akiangazwa kutokana na kumuunga mkono Trump wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais mwaka 2016, pale alionyesha kuwa anafahamu undani wa udukuzi wa takwimu ambao ungeweza kuwafedhehesha Wademokrat, pamoja na hasimu wa Trump katika kinyang'anyiro cha kuingia White House, Hillary Clinton.

Waendesha mashtaka wa Marekani, katika kumkuta anakesi ya kujibu, wamesema kuwa Stone alikuwa ametuma na kupokea barua pepe kadhaa na ujumbe wa SMS wakati wa kampeni mwaka 2016 ambapo alijadili taasisi no 1, mkuu wake, na umiliki wake wa barua pepe zilizo dukuliwa.

XS
SM
MD
LG