Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:24

Cohen adai kuwa Trump hasemi ukweli juu ya kampeni yake


Michael Cohen

Wakili binafsi wa zamani wa Rais wa Marekani Donald Trump, Michael Cohen amesema Ijumaa anaamini kuwa rais hasemi ukweli juu ya suala la kampeni yake kushirikiana na Russia.

Cohen alihukumiwa Jumatano kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, kwa kushiriki kusaidia kufanya malipo kwa wanawake wawili waliokuwa wamedai kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Trump ili wasilizungumze hilo kabla ya uchaguzi wa 2016.

Katika mahojiano yake na shirika la habari la ABC kipindi cha Good Morning America, Cohen alijibu “hapana” alipoulizwa iwapo Trump alikuwa anasema ukweli kwa majibu aliyopeleka kwa Mwendesha Mashtaka maalum Robert Mueller kuhusu masuala yote yanayo husiana na Rashia.”

Cohen amesema ametoa fedha kuwanyamazisha wanawake hao kwa sababu Trump “ alikuwa na wasiwasi kwamba hili jambo litakuwa na athari mbaya katika uchaguzi” iwapo madai haya yangewekwa bayana.

Cohen alijibu, “ bila ya shaka alikuwa anajua” alipoulizwa iwapo Trump alikuwa anafahamu ni kosa kufanya malipo hayo ya kuwanyamazisha wanawake hao, na kuongeza kuwa malipo hayo yalifanyika kumsaidia Trump na kampeni yake.

Cohen alikiri makosa ya kuandaa malipo ya dola za Kimarekani 280,000, kwa kufuata maelekezo ya Trump, kwa nyota mcheza filamu Stormy Daniels na Mwanamitindo wa gazeti la Playboy Karen McDougal. Malipo hayo hata hivyo hayakuwa yameripotiwa kama ni pesa zilizotokana na michango ya kampeni

Cohen pia alikiri kosa la kulidanganya Bunge juu ya juhudi za Trump mapema mwaka 2016 kujenga jumba kubwa la ghorofa Moscow, kwa kuficha madai ya uongo ya Trump aliotoa kwa wapiga kura kwamba hakuwa na ushirika wa biashara yoyote na Russia.

Msemaji msaidizi wa White House Hogan Gidley ametupilia mbali madai ya Cohen katika mahojiano yake, alipoulizwa juu ya hilo na waandishi wanaoripoti ndani ya White House Ijumaa.

“Kwa kweli kwa kuwa vyombo vya habari vinasadikisha kauli ya mtu mhalifu aliyehukumiwa – mnamuamini mtu ambaye amekiri yeye mwenye kwamba ni muongo,” Gidley amesema. “Yeye kusema mimi nitaanza, nitawacha kusema uongo hivi sasa, kuanzia hivi sasa ni jambo la kijinga.”

Trump amepinga suala zima la malipo yaliyo fanyika kuwanyamazisha wanawake hao wawili siyo kitendo cha uhalifu.

Ameliambia kituo cha habari cha Fox News mapema wiki hii kuwa mashtaka yaliyoletwa na waendesha mashtaka “ni kutaka kunifedhehesha. Mimi sikumuelekeza kufanya jambo lolote la makosa au lisilokuwa sahihi.”

XS
SM
MD
LG