Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 02:41

Mcheza filam za ngono adai alitishiwa maisha


FILE - Stormy Daniels alipowasili kwebnye tuzo za 49 za Grammy huko Los Angeles, Feb. 11, 2007.

Mcheza filam za ngono anayedai alikuwa na mahusianio na Rais Donald Trump kabla hajachaguliwa madarakani Stormy Daniels amesema kwamba alitishiwa maisha wakati alipojaribu kueleza hilo.

Ameeleza alikubali kupokea pesa za kumnyamazisha kwa sababu alikuwa akiogopa usalama wa familia yake.

Stormy Daniels ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, alisema katika mahojiano yaliokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa kwamba alikuwa akielekea kwenye darasa lake la mazoezi na mtoto wake mchanga na alifuatwa na mtu asiyemfahamu na kutishwa naye.

Suala hilo lilitokea kwenye eneo la kuegesha magari la Las Vegas 2011 lilitokea muda mfupi baada ya kujaribu kuuza habari hiyo kwa jarida moja mjini humo. Alisema tukio lilimfanya awe mwoga kwa maisha yake kwa miaka kadhaa na alifikiri anafanya jambo lililo bora kwa kukubali dola laki moja na thelathini kutoka kwa wakili wa Trump Michael Cohen ili akae kimya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG