Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:44

Rais mteule akanusha madai juu ya Russia


Donald Trump
Donald Trump

Trump aliandika kuwa ni “HABARI ZA UONGO NA HUJUMA YA KISIASA.”

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump Jumanne usiku kama ilivyo kawaida yake alitumia ukurasa wake wa Twitter kukemea madai kuwa Russia ilikusanya habari katika juhudi za kuharibu sifa zake.

Akitumia herufi kubwa, Trump aliandika kuwa ni “HABARI ZA UONGO NA HUJUMA YA KISIASA.”

Ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari zimesema kuwa nyaraka zilizotolewa na maafisa wa ujasusi zimehusisha tuhuma kuwa baadhi ya maafisa wa kampeni ya Trump walishirikiana na idara za ujasusi za Russia.

Ripoti hiyo pia inasemakana kugusia madai ya tabia za Trump dhulma dhidi ya wanawake. Wakili wa Trump, Michael Cohen hata hivyo amewaambia wanahabari kuwa ripoti hizo zinanuia kumharibia sifa Trump.

XS
SM
MD
LG