WHO imesema, serikali ya Burundi imetangaza kugunduliwa kwa virusi hivyo ambavyo vimekuwa suala la dharura la kitaifa kwa afya ya umma, baada ya visa kuthibitishwa kwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne ambaye alikuwa hajapatiwa chanjo katika wilaya ya Isale magharibi mwa Burundi na watoto wengine wawili ambao walikaribiana naye.
Sampuli nyingine tano kutoka kwa wafuatiliaji wa mazingira ya maji machafu zimethibitisha uwepo wa virusi vya polio aina ya 2 vinayosambaa nchini Burundi, taarifa ya WHO iliongeza
Kuenea kwa virusi vya polio aina ya 2 ni tofauti na vile ambavyo havitokani na chanjo, vikiwa na maambukizi yanayotokea wakati virusi vya polio viliyoko katika chanjo ya mdomo vinapodhoofika na kusambaa miongoni mwa watu ambao hawakupata chanjo kwa muda mrefu.
Ugunduzi ni muhimu wakati vinahusishwa kwanza na matumizi ya chanjo mpya ya mdomo ya aina ya 2 (nOPV2), ambayo haijawahi kutumika, ilitengenezwa hususani kupunguza mambukizi.
Mpango wa Kutokomeza Polio Duniani (GPEI) ulisema katika taarifa kuwa kusambaa kwa virusi vya polio aina ya 2, vinavyotokana na kinga vimegundulika kwa watoto sita katika majimbo ya Kivu Kusini na Tanganyika katika eneo la mashariki mwa DRC
Hata hivyo Burundi ina mpango wa kufanya kampeni ya chanjo ya polio katika wiki zijazo kwa watoto wote wanaostahiki wenye umri wa hadi miaka 7 kwa msaada kutoka WHO na GPEI, WHO ilisema.
Taarifa ya GPEI imesema dozi milioni 600 za chanjo hiyo mpya zimetolewa katika nchi 28 tangu Machi 2021, imerejea kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na yenye ufanisi. DRC imepanga kampeni ya chanjo kufanyika mwezi Aprili
Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters
Facebook Forum