Kundi la watu takribani 250 kutoka jamii ya walio wachache walioteswa huko Myanmar waliwasili katika jimbo la Aceh siku ya Alhamisi, lakini wakaazi waliwaambia wasiingie katika eneo hilo.
Watafiti wamesema kwamba wilaya zilizo katikati mwa Sydney zinakaribia kuwa sehemu za kwanza duniani kufikia lengo la Umoja wa Mataifa, la kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya Ukimwi – HIV.
Shirika la afya duniani WHO, na washirika wake wamesema kwamba karibu dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria duniani, zitatolewa kwa nchi 12 za Afrika ifikapo mwaka 2025.
Siku ya Wakimbizi duniani, ambayo huadhimishwa Juni 20, mwaka huu siku hii inasherehekea ujasiri, uvumilivu, na ushujaa wa mamilioni ya watu ambao wanazikimbia nchi zao ili kuepuka migogoro au mateso.
Rosa Yusif Elias alitoroka Sudan kwa miguu akiwa na watoto wake saba kupitia mpakani kwenda kwenye nchi yake ya Sudan Kusini kwa ajili ya kutafuta usalama.
Kenya itaubadilisha msitu mkubwa wa Shakahola ulioko pwani ya nchi hiyo kuwa kumbukumbu la kitaifa, eneo hilo ambalo miili ya watu zaidi ya 250 ilifukuliwa na kuhusishwa kuwa ni ya wafuasi wa ibada ya siku ya kiyama, waziri mmoja amesema.
Wanaharakati wa kutetea maziringa katika nchi za Afrika mashariki na kati wanayataka makampuni ya kutengeneza vifaa vya kielectroniki na bidhaa za plastiki kuweka utaratibu na kulipia gharama za ukusanyaji na uchakataji wa bidhaa hizo ili kulinda mazingira, viumbe hai na afya za binaadamu.
Mahakama ya Kenya siku ya Ijumaa iliamuru kusimamisha kufukuza kazi kwa wasimamizi wa maudhui kadhaa walioajiriwa na kampuni mkandarasi ya Sama inayofanya kazi na Meta, kampuni mama ya Facebook.
Wakulima wa tumbaku wa mkoa wa Tabora, nchini Tanzania wamesema serikali imeshindwa kutekeleza hatua za kuliondoa zao hilo, na kuwahamashisha wakulima kuingia kweney kilimo cha mazao ya chakula ambayo yataweza kuwaingizia kipato.
Uganda siku ya Jumanne ililaani majibu ya Magharibi kwa sheria mpya dhidi ya ushoga katika taifa hilo la Afrika Mashariki, inayochukuliwa kuwa moja ya sheria kali sana duniani, na kusema vitisho vya vikwazo kutoka kwa wafadhili ni "udanganyifu."
Benki ya Dunia ilisema siku ya Jumanne imeidhinisha mkopo wa dola bilioni moja kwa Kenya ili kusaidia katika bajeti ya taifa hilo kubwa kiuchumi la Afrika Mashariki ambalo linakabiliwa na madeni makubwa na kudhoofika kwa sarafu yake.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema Jumanne kwamba zaidi ya wakimbizi 200,000 nchini Tanzania watapokea nusu tu ya mgao wa chakula kuanzia mwezi ujao kwa sababu ya ukosefu wa ufadhili wa kifedha.
Pandisha zaidi